Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na taratibu za mikopo, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma, yenye kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi 2025.
Wananchi Mbalimbali wakipata elimu kuhusu mambo mbalimbali walipotembelea banda la Wizara hiyo, Sabasaba katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.
Wizara ya Fedha yaibuka Mshindi wa Tatu wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.
Naibu Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akisikiliza maelezo wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo, Sabasaba katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Kitengo cha PPP, Bw. Bashiru Taratibu, akisoma Jarida la Hazina Yetu toleo la Tatu, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Sabasaba.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema (kulia), akikabidhiwa vipeperushi vya huduma zinazotolewa na Kitengo cha Mkataba cha Wizara hiyo na Mkutubi Mwandamizi wa kitengo hicho, Bw. Fredy Mpoma, wakati alipofika kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma.
Afisa kutoka Idara ya Uchambuzi wa Sera Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Fronto Furaha (kushoto), akitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma, kuhusu ripoti ya hali ya Uchumi ya nchi mwaka 2024 kwa wakazi wwa jiji la Dodoma, walipofika kutembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW)
TANZANIA NA JAPAN ZAISAINI MKATABA WA MSAADA WA BILIONI 27.3 KUSAIDIA SEKTA YA AFYA