Frequently Asked Questions
The United Republic of Tanzania
Ministry of Finance
Treasury Square Building 18 Jakaya Kikwete Road
P.O.BOX 2802,
40468 Dodoma.
Email Address
Phone
Please use the feedback form obtained in contact us section.
How Service FProviders (SPs) can join GePG?
Two Cases to join GePG.
For Service Providers (SPs) with Billing Systems these are steps to join GePG
- Fill the GePG Registration (SP and Admin User from SP) Form that are provided by Ministry of Finance (GePG).
- Integrate the Billing system with GePG according to required standard (API) provided by Ministry of Finance.
- Conduct and present Test case Result to GePG for decision making.
- Prepare training to all GePG users with its cost incurred by SP facilitated by one or two facilitators from Ministry of Finance.
- Present Bank Account details for both commercial banks as well as in Bank of Tanzania.
- Prepare Revenue Sources and Targets
- Prepare Revenue Collection Centers
- Prepare two ICT officers who will be responsible to manage GeFG. system.
For Service Providers (SPs) without Billing Systems these are steps to join GePG
- Fill the GePG Registration Form that are provided by GePG.
- Prepare Training Budget for GePG System that its cost will be incurred by SP.
- Present Bank Account details for both commercial banks as well as in Bank of Tanzania.
- Prepare Revenue Sources and Targets
- Prepare Revenue Collection Centers
- Prepare two ICT officers who will be responsible to manage GePG. system.
- PSPs Write the application letter to Permanent Secretary, Ministry of Finance requesting to join GepG.
- Ministry of Finance (GePG) after receiving the application logs the request and Call PSPS for Sensitization session.
- Request is forwarded to Procurement Department for processing
- PSP are engaged by procurement.
- Once procurement process has initiated, PSPs are given technical details and requirements for testing environment.
- Once internal procurement process has been completed, PSPs are informed and to sign a standard contract for engagement of service providers for facilitating integration to GePG.
- Integration to live environment starts after signed a standard contract.
Wizara ya Fedha ina jukumu la kusimamia shughuli za uendeshaji wa minada kwa mujibu wa Kifungu cha 6 cha Sheria ya Waendesha Minada, Sura ya 227, ilitungwa na kuanza kutumika mwaka 1928 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1930, 1994 na 2002.
Leseni hizi zimekuwa zikitumiwa katika uendeshaji wa minada ya hadhara, ukusanyaji wa madeni, ushuru, tozo, udalali wa mahakama, udalali wa nyumba, viwanja, n.k.
Leseni hizi hutolewa kwa Kipindi cha Mwaka mmoja au nusu mwaka (miezi sita) kwa kufuata mwaka wa Kalenda (Januari hadi Disemba kwa gharama ya shilingi 150, 000/=, Januari hadi Juni au Julai hadi Disemba kwa gharama ya shilingi 75,000/=).
Ili mwombaji aweze kupewa Leseni anatakiwa kujaza fomu ya maombi ambayo ni lazima ithibitishwe na Katibu Tawala wa Wilaya anakofanyia Biashara.
Fomu ya maombi ya Leseni iliyojazwa kikamilifu huwasilishwa ikiwa na viambatisho vifuatavyo:-
- Tax Clearance Certificate ambayo hutolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
- Nakala ya Hati ya Usajili wa Biashara inayotolewa na BRELA.
- Nakala ya Leseni ya Biashara inayotolewa na Halmashauri/Manispaa
- Nakala ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)
Mwombaji wa Leseni ataingia katika tovuti ya Wizara ya Fedha (www.mof.go.tz) na kisha kuponyeza GAMIS Portal kwenye Quick Links.
Kujisajili mara ya kwanza bonyeza Create Account.Jaza taarifa zinazohitajika kwenye ukurasa wa Registration kisha bonyeza Register.
Ili kufanya maombi ingia kwenye Mfumo bonyeza Auctioneer kisha bonyeza +Add Auctioneer Licence. Kwenye ukurasa wa Add Auctioneer Licence jaza kikamilifu Taarifa zinazohitajika.
Baada ya kukamilisha usajili na kuingia (Sign in) kwenye mfumo Bonyeza Documents ili kupakua (download) fomu ya Maombi (Application Form).
Baada ya kupakua Fomu ya maombi, mwombaji atapaswa kuijaza kikamilifu na kuiwasilisha kwa katibu Tawala wa Wilaya kwa ajili ya Uhakiki na Saini.
Vile vile, Mwombaji anapaswa kuhakikisha kuwa na nyaraka zifuatazo ;-
- Tax Clrealance Certificate inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA);
- Certificate of Corporation/Incorporation zinazotolewa na BRELA;
- Leseni ya Biashara inayotolewa na Halmashauri/Manispaa;
- Nakala ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)
Mwombaji atapaswa kuzi scan nyaraka hizi ili aweze kuzi – attach kwenye Mfumo.
Bonyeza Choose File ku – attach Nyaraka katika chumba husika na kisha Bonyeza Save kwenda hatua inayofuata.
NB: Kumbuka kuwa kwenye Usajili zinaingizwa taarifa za Mtu kwa niaba ya Kampuni, lakini kwenye ukurasa huu JAZA TAARIFA ZA KAMPUNI NA SIO MTU.
Mfumo wa GAMIS Portal unaonyesha Status ya Maombi ya Leseni kama ifuatavyo ;-
- Requested – Maombi yametumwa
- Rejected – Maombi yamekataliwa
- Awaiting for Payment -Fanya malipo
- Paid – Malipo yamekamilika
Iwapo maombi yako yamekataliwa (Rejected) bonyeza Details kuona sababu za maombi kukataliwa. Bonyeza Edit kufanya marekebisho na kisha wasilisha upya maombi (Re – Submit).
Mfumo wa GAMIS Portal umeunganishwa na Mfumo wa Malipo wa Serikali wa GePG. Baada ya maombi kukubaliwa mwombaji atapewa control Number na maelekezo ya kufanya malipo. Bonyeza Datalis kupata Control Number.
Malipo haya yanaweza kufanyika kwa njia ya Benki, Mawakala au Mitandao ya Simu.
Malipo haya yanapaswa kukamilishwa ndani ya Siku Thelathini (30). Endapo mwombaji hatalipa ndani ya siku hizo anapaswa kuomba upya control number kwa ajili ya kufanya malipo husika.
Baada ya kukamilisha malipo Mwombaji atafika katika Ofisi ya Msimamizi wa Mali za Serikali ya Mkoa alipo kwa ajili ya kuchukua Leseni yake.
Mwombaji atapaswa kwenda na nyaraka halisi alizoziambatisha wakati wa kuwasilisha Maombi. Mwombaji hatapewa Leseni yake iwapo hatakwenda na nyaraka husika au ikionekana kuna Tofauti kati ya nyaraka alizoziambatisha na nyaraka halisi, nyaraka anazopaswa kwenda nazo ni; -
- Fomu ya Maombi;
- Tax Clearance Certificate;
- Certificate of Registration/Incorporation; na
- Leseni ya Biashara.
Mwombaji anapaswa kuomba kibali cha kusajili chombo husika kwa kuwasilisha maombi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha likiambatana na nyaraka zifuatazo;
- Mkatataba wa mauzo uliotolewa wakati wa mnada
- Uthibitisho wa malipo yaliyofanyika kwa ununuzi wa chombo husika
- Taarifa ya ukaguzi (Vehicle Inspection report) kutoka Jeshi la Polisi inayoonesha ubora wa gari kuweza kutumika (Road worthness).
Baada ya kujiridhisha na taarifa hizo zilizowasilishwa, Wizara ya Fedha hutoa ridhaa ya usajili wa chombo husika kwa kuijulisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iweze kuendelea na taratibu za usajili wa chombo hicho