Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. BALOZI OMAR AZINDUA OFISI ZA TRA ZINAZOTEMBEA

27 Feb, 2026
MHE. BALOZI OMAR AZINDUA OFISI ZA TRA ZINAZOTEMBEA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), leo tarehe 25 Februari 2026, amezindua Ofisi zinazotembea (Magari Maalum) mawili katika maeneo ya kibiashara ya Mwenge na Tegeta, Jijini Dar es Salaam, yatakayotumiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhudumia wateja (Walipakodi) katika maeneo mbalimbali nchini.

Magari hayo maalumu ni sehemu ya magari kumi ya aina hiyo ambayo Serikali Kupitia Wizara ya Fedha, imeipatia TRA wa ajili ya kuwahudumia wananchi hususan katika maeneo ambayo Walipakodi watakuwa na changamoto ya kutumia mifumo ya TEHAMA ya TRA ya masuala ya kodi kutokana na ukosefu wa mtandao wa Intaneti.

Akizungumza na Wananchi pamoja na walipa kodi kwa nyakati tofauti katika eneo la Mwenge na Tegeta, Jijijni Dar es Salaam, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, aliwataka watumie huduma hiyo ipasavyo kwa ajili ya masuala ya kikodi ikiwemo kuomba ushauri wa namna bora ya kulipa kodi.

Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu wa Walipakodi ndiyo sababu imeamua kuwekeza katika vitendea kazi hivyo vitakavyo warahisishia ufanisi wa ulipaji kodi na huduma za kikodi kwa wananchi.

Akijibu baadhi ya maombi, ushauri na maoni ya wananchi, katika maeneo hayo, Mhe. Balozi Omar alisema kuwa kwa maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suuhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kupitia Bajeti Kuu itakayosomwa Bungeni mwezi Juni mwaka huu, Serikali inatarajia kuongeza kiwango cha fedha zinazopelekwa TAMISEMI kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na Watu wenye mahitaji maalumu kutoka asilimia 10 za sasa hadi kufikia asilimia 15, ili kiasi cha fedha kitakachoongezwa kitumike kuboresha miundombinu ya kuwawezesha wananchi kufanya biashara zao yakiwemo Masoko.

Alielezea kufurahishwa kwake na maoni yaliyotolewa na wananchi kila mahali alipopita kuhusu uhusiano mzuri uliopo kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Walipakodi na kutaka uhusiano huo uendelee na kuwahimiza wananchi waendelee kulipa kodi kwa hiari kwa ajili ya kuiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake ya kuiletea nchi maendeleo kwa ufanisi zaidi.

Mhe. Balozi Omar kwa nyakati tofauti alizungumza na baadhi ya wafanyabiashara katika maeneo hayo, ambapo aliwataka watumie huduma hiyo ipasanyo kwa ajili ya masuala ya kikodi ikiwemo kuomba ushauri wa namna bora ya kulipa kodi.

MWISHO