Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MWAMBA AKABIDHIWA JARIDA LA HAZINA YETU TOLEO LA TATU

27 Jun, 2025
DKT. MWAMBA AKABIDHIWA JARIDA LA HAZINA YETU TOLEO LA TATU

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akikabidhiwa Jarida la ‘’Hazina Yetu’’ Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo amekipongeza Kitengo hicho kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutangaza na kuhabarisha umma kuhusu Sera, Program, Mikakati na Mipango mbalimbali inayofanywa na Wizara katika kusimamia uchumi wa nchi.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba, amepokea Jarida la Hazina Yetu Toleo la Tatu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 linaloandaliwa na Wizara kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kila baada ya miezi mitatu.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Jarida hilo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, Katibu Mkuu, Dkt. Mwamba, alipongeza kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Kitengo hicho katika kuhabarisha umma kuhusu Sera, Program, Mikakati na Mipango mbalimbali inayofanywa na Wizara katika kusimamia uchumi wa nchi na kwa kuandaa Jarida hilo katika viwango vya hali ya juu.

Aliahidi kuwa Wizara itaendelea kikiwezesha Kitengo hicho ili kiongeze vifaa vya kisasa vya kukusanya, kuchakata na kusambaza habari kwa wadau mbalimbali wa wizara walioko ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Jarida la “Hazina yetu”limesheheni maarifa mbalimbali kupitia makala, habari, matukio, habari picha na matangazo mbalimbali na husambazwa kwa njia ya nakala ngumu (hard copies) na nakala tete (soft copies) kupitia mitandao ya kijamii ya Wizara na wadau wengine wa habari pamoja na Tovuti ya Wizara ya Fedha www.mof.go.tz 

Mwisho.