Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

Tanzania yapokea msaada wa Shilingi bilioni 68 kutoka Ujerumani

06 Nov, 2021 Download

Tanzania imepokea msaada wa Euro milioni 25 sawa na shilingi bilioni 67.82 kutoka Serikali ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo ya KfW, kwa ajili ya mradi wa Uhifadhi endelevu wa Maliasili na Mifumo ya Ikolojia nchini. Mkataba wa msaada huo umesainiwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) wa Umoja wa Afrika, Bw. Christoph Tiskens, kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani.