Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

BENKI YA DUNIA YAIMWAGIA TANZANIA SHILINGI TRILIONI 1.8 KUKUZA UCHUMI NA KUBORESHA SEKTA YA AFYA

22 Dec, 2022 Download

DODOMA, 22 Desemba, 2022 – BENKI ya Dunia imeiidhinishia Tanzania, mkopo wenye masharti nafuu pamoja na msaada vyote vikiwa na thamani ya dola za Marekani milioni 775 (Sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 1.8), kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa bajeti, kuboresha uchumi na huduma za afya.

Mchanganuo wa fedha hizo unaonesha kuwa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (IDA) litatoa mkopo wa dola za Marekani milioni 500 (sawa na shilingi trilioni 1.1) kwa ajili ya kufufua uchumi ulioathiriwa na UVIKO-19 na Vita vinavyoendelea baina ya Ukraine na Urusi, vilivyosababisha kusinyaa kwa shughuli za kiuchumi na kupanda kwa bei ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje yakiwemo mafuta na bidhaa nyingine.