Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA YAZIASA TAASISI ZA SERIKALI KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO YA UKOPAJI, MISAADA NA DHAMANA

14 Aug, 2024
WIZARA YA FEDHA YAZIASA TAASISI ZA SERIKALI KUFUATA SHERIA NA MIONGOZO YA UKOPAJI, MISAADA NA DHAMANA
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, akifungua magunzo na Elimu kwa Taasisi za Serikali, kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134 na Miongozo mbalimbali kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo, kwa Niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa  itawajengea uwezo taasisi hizo ili kifuata sheria hiyo inauompa mamlaka Waziri wa Fedha kusimamia mikopo, dhamana na misaada ambayo nchi inapata kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kutekelezaji miradi ya maendeleo.
 
Wizara ya Fedha imezitaka Taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa zinafuata Sheria na Miongozo ya ukopaji fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na taasisi hizo.
 
Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Wizara ya Fedha, Bwana Omary Khama, wakati akifungua kikao kazi cha siku mbili kwa Taasisi za Serikali kuhusu matakwa ya Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada namba 134 pamoja na miongozo mbalimbali katika kufadhili miradi ya maendeleo.
 
Alisema kuwa hatua hiyo inachukuliwa ili kuhakikisha kuwa matakwa  ya Sheria hiyo inayoelekeza kuwa mwenye dhamana ya kukopa kuweka dhamana na kupokea misaada ni Waziri wa Fedha.
 
Alifafanua kuwa ni lazima Taasisi ziandae maandiko ya miradi ikihusisha upembuzi yakinifu, kuwa na timu mahiri za kusimamia miradi pamoja na Wizara husika kutenga bajeti ya kutekeleza miradi husika kwa ufanisi.
 
Bw. Khama alisema kuwa Sheria namba 134 ya Mikopo, Dhamana na Misaada, imelenga kuhakikisha kuwa Serikali inakopa mikopo yenye gharama nafuu pamoja na kuepuka masharti hası ya mikopo husika.
 
Wizara ya Fedha  inatoa mafunzo kuhusu vipengele mbalimbali vya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na taratibu na mazingatio yanayohusiana na Sheria ya mikopo, dhamana na misaada Sura ya 134, pamoja na mwongozo wa utambuzi wa miradi, uandaaji, utekelezaji, na majadiliano ya mikopo na misaada kwa ajili ya kufadhili miradi ya maendeleo.
 
“Mwongozo una lengo la kusaidia maendeleo ya masoko ya kifedha ya ndani na nje na kuhakikisha kuwa madeni yasiyo ya lazima yanaepukwa”
 
MWISHO