Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA YATWAA TUZO MAONESHO YA 49 YA SABASABA

08 Jul, 2025
WIZARA YA FEDHA YATWAA TUZO MAONESHO YA 49 YA SABASABA
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Kulia), akimkabidhi tuzo Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhan Kissimba, baada ya Wizara ya Fedha kuibuka Mshindi wa Tatu wa Jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Kilwa Road, Jijini Dar es Salaam.
 
Wizara ya Fedha imeibuka na tuzo ya Mshindi wa Tatu wa jumla kwa upande wa Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
 
Tuzo hizo zimetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jaffo ambapo kwa upande wa Wizara ya Fedha Tuzo hiyo imepokelewa na Afisa Habari Mwandamizi, Bw. Ramadhan Kissimba, kwa niaba ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Benny Mwaipaja, ambapo ushindi huo umetokana na Wizara zilizotoa huduma bora kwa wananchi katika Maonesho hayo.
 
Wizara ya Fedha inatoa huduma katika Maonesho hayo kupitia Idara, Vitengo na Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha ikiwa ni pamoja na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji Tanzania (UTT AMIS), Mfuko wa Self Microfinance, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
 
Taasisi nyingine ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Baraza la Masoko ya Mitaji (CMT), Benki ya Maendeleo TIB na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Hazina SACCOS, Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) na Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
 
Mwisho.