Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA YAJINOA UTOAJI WA TAARIFA KWA UMMA

10 Sep, 2025
WIZARA YA FEDHA YAJINOA UTOAJI WA TAARIFA KWA UMMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano Wizara ya Fedha, baada ya kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kuwa sehemu ya kufanikisha utoaji taarifa sahihi na kwa wakati kwa umma ili kutimiza haki ya wananchi kupata taarifa.

Rai hiyo imetolewa jijini Dodoma wakati wa Kikao kazi cha Kamati hiyo kinachohusisha wajumbe kutoka Idara na Vitengo vya Wizara kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa matumizi ya umma.

Bw. Mwaipaja alisema kuwa Wizara ina jukumu la kutoa taarifa kwa umma kuhusu sera, program, mipango na matukio ya Wizara ili kuuwezesha umma kuwa na uelewa kuhusu majukumu ya Wizara na mambo mengine.

“Nitoe rai kwa wajumbe wa Kamati hii kuhakikisha mnatoa ushirikiano kwa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa kuainisha kalenda za matukio muhimu kwa umma ili kitengo kiweze kuzifanyia kazi”, alisema Bw. Mwaipaja.

Alisema taarifa zinazopatikana hutumika kuandaa majarida ya Wizara lakini pia kuwezesha kutoa taarifa kupitia Tovuti ya Wizara, Instagram, Whatsap, Tweeter, Linkidin Hazina Tv na vyombo vingine vya Habari kama runinga na magazeti.

Alisema kuwa tayari Wizara imetoa Jarida la Hazina Yetu Toleo la Nne ambalo limesheheni taarifa muhimu kwa umma na inaendelea na kuandaa Toleo la Tano ambalo linategemea taarifa zilizopo katika Idara na Vitengo vya Wizara.

Alisema kuwa kupitia chaneli mbalimbali za mawasiliano ambazo Wizara hutumia kuwasilisha Majarida hayo, kuna wadau ambao wanahitaji kuendelea kutoa taarifa kwa kuwa zinaandaliwa kwa lugha nyepesi yenye kueleweka kwa watu mbalimbali.

Aidha, amewataka wajumbe hao kuendelea kuhamasisha wadau wa ndani na nje kufuatilia taarifa zinazotolewa na Wizara kwa manufaa yao katika  kuongeza maarifa na matumizi mengine ya tafiti za kitaaluma.

Mwisho.