Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA NI MDAU MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI DIRA 2050

09 Jul, 2025
WIZARA YA FEDHA NI MDAU MUHIMU KATIKA UTEKELEZAJI DIRA 2050

Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, akipewa maelezo na Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Amri Matole, kuhusu takwimu rasmi na mchango wake katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

 

Tume ya Mipango itaendelea kushirikiana na Wizara ya Fedha na Taasisi zake katika utekelezaji na ufuatiliaji wa Dira ya Maendeleo 2050 kwa kuwa kazi nyingi za Tume hiyo zinategemea  matokeo ya kazi zinazofanywa na Wizara hususani Ofisi ya Taifa ya Takwimu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, 

alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa Takwimu mbalimbali za kiuchumi, kijamii na mazingira zitasaidia katika kupanga, kupima, kufuatilia na kufanya tathmini ya  programu za maendeleo wakati wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

Dkt. Msemwa alisema kuwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050,Tume itahitaji takwimu na viashiria muhimu  vya mara kwa mara kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikiwa ni pamoja na takwimu rasmi katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya  idadi ya watu, pato la taifa na viasihiria vingine vya kiuchumi na kijamii ukiwemo  mfumuko wa bei. 

Aidha, viongozi mbalimbali wa Taasisi na Idara wameendelea kutembelea Banda la Wizara ya Fedha akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Joseph Kuzilwa.

Viongozi wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Prof. Geradine Rasheli, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza na Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Ruth Minja.  

Wengine ni Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William Pallangyo, Kaimu Mkurugenzi wa TIB Development Bank, Joseph Chilambo, Mkurugenzi wa Hazina Saccos, Dkt. Festo Mwaipaja, Msajili Baraza la Masoko ya Mitaji, Bw. Martin Kolikoli na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Dkt. Kedmon Mapama.

Wizara ya Fedha kupitia Idara na Vitengo lakini pia Taasisi zilizo chini ya Wizara, inaendelea kuwakaribisha watanzania kutembelea Banda la Wizara hiyo ili waweze kuhudumiwa. 

Mwisho.