Category Title

  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Economic Survey Books
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WIZARA YA FEDHA KUBORESHA MTIRIRIKO WA MAJUKUMU

15 Aug, 2022
WIZARA YA FEDHA KUBORESHA MTIRIRIKO WA MAJUKUMU

Naibu Katibu Mkuu Huduma za Hazina wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Omolo, amewataka wataalam wa Idara na Vitengo vya Wizara hiyo kuhakikisha wanapitia kwa umakini mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu ya Wizara na kuuboresha ili uweze kuleta tija katika utoaji huduma bora na kwa wakati kwa manufaa ya Taifa.

Rai hiyo imetolewa mkoani Singida wakati akizungumza na timu ya wataalam wa wizara hiyo ambayo inapitia mtiririko wa hatua za utekelezaji wa majukumu na kuuboresha ili uweze kuwa na ufanisi.

Alisema kuwa ni vema Wizara ya Fedha na Mipango ikaonesha mfano wa kiutendaji wenye tija katika masuala ya mipango, uchumi, sera na usimamizi wa fedha na kuondoa utaratibu ambao hauna tija kwa wizara, Taifa na wananchi kwa ujumla.

Alisema wizara hiyo inapofanya kazi kwa ufanisi inachochea maendeleo ya kiuchumi katika sekta nyingine na kutimiza lengo la Serikali la kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa.

Mwisho.