Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WAZIRI WA FEDHA ATETA NA MABALOZI

20 Feb, 2026
WAZIRI WA FEDHA ATETA NA MABALOZI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Balozi wa Uingereza Mhe. Marianne Young baada ya mkutano kati yao kuhusu ushirikiano wa Maendeleo, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza Mhe. Marianne Young pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Waziri alisisitiza dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuimarisha sekta mbalimbali, hususan zile zinazogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

Alibainisha kuwa ushirikiano wa nchi na nchi ni chachu ya kufanikisha miradi ya maendeleo na kuongeza ustawi wa kijamii na kiuchumi.

Aidha, Mhe. Balozi Omar, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kufanya shughuli zake kwa uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku akiwahakikishia washirika wa maendeleo kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana kwa dhati ili kufanikisha malengo ya pamoja.

Kwa upande wao, Mabalozi wa Uingereza na Sweden walieleza kuwa nchi zao zinathamini uhusiano wa muda mrefu na Tanzania na wataendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Melckzedeck Mbise na Wajumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza na Sweden.

Mwisho.