Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA MIIKO NA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

24 Jun, 2025
WATUMISHI WAASWA KUZINGATIA MIIKO NA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza wakati wa kilele cha   Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

 

Watumishi wa Umma wameaswa kuendelea kuzingatia miiko na maadili ya utumishi wa umma, sera za nchi, sheria, kanuni na miongozo iliyopo; ambayo inahitaji ukarimu, kuwapokea, kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Maelekezo hayo yametolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) alipokuwa akihitimisha kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na Uzinduzi wa Mifumo ya Kidijiti kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Mhe. Majaliwa alisema ni vyema kuimarisha mikakati ya kuhamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kutumia fursa za uwepo wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma ili wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata huduma zinazotolewa na Serikali kwa haraka zaidi.

Wakati akizindua mfumo wa Kidijiti Mhe Majaliwa, alizitaka Taasisi zote za umma kutekeleza agizo la Mhe Rais,  Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kuwa Taasisi zenye mifumo na zinazoendelea kubuni mifumo inasomana na zinaweza kubadilishana taarifa kupitia mfumo huo ili kuboresha huduma ndani ya Serikali.

“Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA hakikisheni kwamba mifumo iliyounganishwa inendelea na majukumu yake ya kubadilishana taarifa lakini pia kila anaeingia mjiridhishe kuwa ana uwezo wa kuwasiliana na yeyote alioko kwenye mfumo. Alisema Mhe. Majaliwa.

Vile vile Mhe. Majaliwa aliwaasa watumishi wa umma kote nchini kujisajili katika mfumo wa kidijitali wa e – wezesha, ambao unawezesha watumishi wa umma kuwekeza moja kwa moja kupitia makato ya mshahara au mapato mbalimbali ya biashara.

Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, ambayo yalianza tarehe 16 Juni, 2025 na kuhitimishwa leo tarehe 23 Juni, 2025  yameshirikisha Taasisi za Serikali 146, ikiwemo Wizara ya Fedha, pamoja na wafanyabiashara wa makundi mbalimbali

Mwisho.