Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WAHITIMISHA TAMASHA LA PASAKA

02 Apr, 2024
WATUMISHI WA WIZARA YA FEDHA WAHITIMISHA TAMASHA LA PASAKA
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda (aliyesimama), akizungumza na watumshi wa Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, (hawapo pichani), katika hafla ya kuagana iliyofanyika katika ukumbi wa ‘Golden Crown’ Jijini Dodoma, mara baada ya kukamilisha Tamasha la Pasaka lilioambatana na Bonanza la michezo na kukamilishwa na matendo ya huruma kwa kutembelea na kugawa misaada ya vyakula, fedha, na mahitaji mengine katika vituo mbali mbali vya watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo kituo cha Safina, Asmaa Bint Shams kilichopo kisasa, kituo cha wasiooa watu wazima Buigiri na kituo cha watoto wenye uhitaji maalum Shule ya Msingi Buigiri.
 
Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Ofisi ya Rais Fedha na MipangoZanzibar kwa Mwaka 2024, limehitimishwa baada ya watumishi wa Wizara ya Fedha pande zote mbili za Muungano kukamilisha zoezi la kutoa misaada kwa vituo mbalimbali vya watu wenye uhitaji maalum na vituo vya watoto yatima.
 
Akizungumza katika hafla ya kuagana na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa’ Golden Crown’ jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda, aliwashukuru watumishi wote wa pande zote mbili kwa ushiriki wao katika Tamasha hilo huku akiahidi kufanyika kwa tukio kama hilo mwakani.
 
“Nimefurahi sana na nawashukuru kwa ushiriki wenu, msafiri salama na endapo kutakuwa na changamoto yoyote tunaomba mtufahamishe, tuna ofisi sehemu mbalimbali ikiwemo Dar Es Salaam na maeneo mengine hapa nchini hivyo ni rahisi kusaidia ikiwa kutatokea changamoto yoyote ‘’ Alisema Bw. Mwenda
 
Kwa upande wake, Afisa Uendeshaji kutoka Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Rajab Uweje, akizungumzia kuhusu ziara ya kutembelea vituo vya watu wenye uhitaji, aliainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye mahitaji maalum na vituo vya kulelea watoto yatima ikiwemo makazi na fedha za kujiendesha.
 
‘’Tumeona changamoto nyingi za vituo hivi mfano kituo cha Safina kina uhitaji wa pampu za kusukuma maji ambazo matengenezo yote yanagharimu kiasi cha shilingi milioni saba na nusu na tumewapa milioni moja tu’’ alisema Bw. Uweje
 
Aliongeza kuwa Ofisi ya Rais Fedha na Mipago Zanzibar itashirikiana na Wizara ya Fedha Tanzania Bara ili kuona namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye mahitaji maalumu katika vituo hivyo katika awamu nyingine.
 
"Na tumetoa ahadi kuwa tumechukua zile changamoto zao ili tuone tunaenda kuzifanyia kazi vipi, endapo tutafanikiwa kuwa mshawishi viongozi wetu katika Taasisi zetu basi tutarudi na kuona tutawasaidia vipi"Aliongeza Bw. Uweje.
 
Aidha, alitoa wito kwa walezi wanaohudumia watu wenye mahitaji maalumu ikiwemo Watoto yatima kuwalea katika malezi bora ili wasione utofauti na watu wengine ikiwa ni pamoja na kuwasimamia katika masomo yao na kuwapa misingi bora ya kiimani kwa kila mmoja kutokana na dini yake.
 
"Wito wangu kwa walezi wa vituo waendelee kuwatunza watoto hawa, kuwasimamia vizuri ili muwe na mchango bora kwa Taifa na raia wema wa leo na baadae" alisisitiza Bw. Uweje.
 
Kila mwaka Watumishi wa Wizara ya Fedha na Watumishi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar hutembelea vituo mbalimbali na kufanya matendo ya huruma katika maeneo yote mawili kwa zamu (Tanzania Bara na Zanzibar) ambapo kwa mwaka huu wametembelea Vituo vya Safina, Asmaa Bint Shams kilichopo kisasa, kituo cha watu wazima (wakubwa) wasioona Buigiri na Kituo cha Watoto wenye uhitaji maalum kilichopo Shule ya Msingi Buigiri na kutoa misaada ya vitu mbalimbai ikiwemo vyakula, sabuni, mafuta, dawa za meno, fedha na mahitaji mengine.
 
Mwisho.