Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA NA UHUSIANO ULIOPO KATI YA WASHIRIKA NA SERIKALI

01 Mar, 2024
WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA NA UHUSIANO ULIOPO KATI YA WASHIRIKA NA SERIKALI
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akihutubia wakati wa Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati wa Ngazi ya Juu 2024, wenye kaulimbiu,”Kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; Kuongeza Kasi ya Uchumi Himilivu na Maendeleo Jumuishi katika Nyakati Zisizotabirika, uliohusisha Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na Asasi Zisizo za Kiserikali, katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha nchi inakuwa na maendeleo endelevu.
 
Dkt. Nchemba alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo ngazi ya Juu.
 
Alisema kuwa Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuwa na maendeleo endelevu ambayo hayamuachi Mtanzania yoyote nyuma kwa kufanya uwekezaji katika Sekta za Uzalishaji.
 
“Kipaumbele kimewekwa kwenye uwekezaji katika mtaji wa binadamu, maendeleo ya miundombinu, kuhamasisha ukuaji wa kiuchumi, kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii, utawala bora, kuwawezesha wanawake na uhifadhi wa mazingira”, alibainisha Mhe. Nchemba.
 
Alisema kuwa kwa kutekeleza mikakati hiyo pamoja na kukuza ushirikiano na sekta binafsi, asasi za kiraia na washirika wa maendeleo, Tanzania inaweza kupiga hatua kubwa kuelekea kufikia ukuaji wa Uchumi endelevu.
 
Dkt. Nchemba alisema Serikali inatambua umuhimu wa kuimarisha mazingira ya ukuaji wa biashara, kuongeza ushindani na kukuza ubunifu ili kukuza uchumi wa nchi.
 
Aidha, Dkt. Nchemba, alisema Tanzania pia inatumia Diplomasia ya Kiuchumi kama mkakati muhimu wa kuendeleza uchumi wake na kubainisha kuwa nchi ina dhamira kubwa ya kufuata kanuni za ushirikiano wa kimataifa wenye manufaa kwa pande zote.
 
Kwa upande wake, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. David Concar, alisema kuwa wadau wa maendeleo wanampongeza Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoyafanya na wanayaona mabadiliko mbalimbali anayofanya katika kuboresha mazingira ya uwekezaji, biashara pamoja na uwekezaji katika sekta ya uzalishaji.
 
Alisema kuwa wadau wa maendeleo wako tayari kuendelea kuiwezesha nchi kufikia maendeleo ya kukuza uchumi wa wananchi.
 
Mhe. Concar alisema  wadau wa maendeleo wametoa zaidi ya Dola bilioni 2.7 kwa ajili ya kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo asilimia 51 ya fedha hizo ni misaada na asilimia 49  ni mikopo yenye masharti nafuu.
 
Alibainisha kuwa asilimia 40 ya fedha hizo zilitolewa na nchi moja moja za washirika wa maendeleo na asilimia 60 za fedha hizo zimetolewa na Taasisi za Kimataifa za fedha ikiwemo  Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa  (IMF)
 
Nao washiriki wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SRF, Prof. Fortunata Makene na Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Dk. Donald Mmari, walisema kuwa majadiliano hayo ni muhimu kwa maendelo ya nchi kwa kuwa yanaikutanisha Serikali na wadau wa maendeleo.
 
Mwisho.