Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WAKUU WA VITENGO VYA MAWASILIANO WAASWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI

25 Oct, 2023
WAKUU WA VITENGO VYA MAWASILIANO WAASWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano la Wahariri wa vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi Maafisa Mawasiliano/ Masoko na Wahariri, kutumia kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla.
 
Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano vya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, wameaswa kuendelea kutangaza majukumu yanayofanywa na taasisi zao kikamilifu ili kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu miradi ama kazi zinazotekelezwa na Taasisi hizo na kuchangia kukuza uchumi na maendeleo ya nchi.
 
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati akifungua Kongamano la Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano na Masoko vya Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari lililofanyika katika Ukumbi wa Nanenane, Mkoani Morogoro.
 
Aliwasisitiza Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano wote kutumia jukwaa hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa kwa wadau, na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi utakaoongeza ufanisi katika utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla. 
 
Bi. Omolo alifafanua kuwa Mawasiliano ndio msingi wa mafanikio wa kila jambo, na kupitia mawasiliano Taarifa njema zinazohusu Taasisi zinaweza kusomwa na Wadau mbalimbali wa ndani na nje   na kuelewa mambo mazuri wanayoyatekeleza, hivyo wana wajibu wa kuhakikisha  kuwa wanazingatia Mawasiliano imara ya kimkakati ili kujenga Taswira chanya  kwa Wizara, Taasisi na Taifa kwa ujumla.
 
Alisema kuwa lengo kuu la kongamano hilo lilikuwa kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa kwa wadau zinazohusu Wizara na Taasisi zake.
 
“Nimefarijika sana kuona kwamba mmeitikia wito wa kushiriki katika Kongamano hili, hii ni ishara njema kwa ustawi wa Wizara na Taasisi zake katika kukuza na kuimarisha Mawasiliano kwa Umma. Ni matumaini yangu kuwa siku za usoni kongamano hili litakuwa ni miongoni mwa makongamano bora na makubwa zaidi nchini” alisema Bi. Omolo.
 
Awali, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, aliwapongeza Wahariri na vyombo vya habari nchini kwa namna zinavyosukuma agenda ya Maendeleo na kutangaza habari zinazochagiza ukuaji wa uchumi wa nchi na kuifanya Tanzania iwe kinara katika Usimamizi na ukuaji wa uchumi katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.
 
Alisema kuwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, limesifu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kusimamia uchumi na Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa nchi inasimamia sera zake za uchumi na fedha kwa umahili
 
Naye Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wa Kongamano hilo, Bw. Ben Mwang'onda, aliishukuru Wizara ya Fedha kwa kuandaa kongamano hilo ambalo limekua daraja la mahusiano kati ya Wizara hiyo na Umma katika kutoa taarifa mbalimbali. 
 
Hilo ni Kongamano la pili la Mawasiliano kufanyika kati ya Wizara ya Fedha na Taasisi zilizo chini yake ambazo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Soko la Bidhaa Tanzania-TMX, Chuo cha Uhasibu Arusha-IAA, Mfuko wa Self-SELF Microfinance, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini - IRDP, Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma - PPAA, Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini - GPSA, Mfuko wa Uwekezaji - UTT-AMIS, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi - PSPTB, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma - PPRA, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania - TIRA, Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika - EASTC, Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB, Hazina Saccos na Shirika la Bima la Taifa – NIC.
 
 
Mwisho