Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

WAKAZI WA KASELYA WILAYANI IRAMBA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI

07 Dec, 2022
WAKAZI WA KASELYA WILAYANI IRAMBA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI

WAKAZI wa Kata ya Kaselya Wilayani Iramba mkoani Singida wameondoka na na adha ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa Maji wa Kaselya uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 770.

Wakazi hao wameishukuru Serikali kwa kufanikisha na kukamilisha ujenzi wa mradi huo, wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipotembelea na kukagua mradi huo ambao fedha zake zinatokana na mradi wa kukabiliana na athari za UVIKO 19.

“Tunakuomba utupelekee salam nyingi kwa Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kututatulia changamoto ya maji kafika kata yetu, ametutua ndoo kichwani wanawake na wewe Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wetu kwa jitihada zako za kufanikisha mradi huu na miradi mingine” walisema wakazi wa kata hiyo

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba aliahidi kumfikishia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pongezi za wananchi hao kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo kwa kasi kubwa.

Alisema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akipigiwa mfano na mashirika ya Fedha ya Kimataifa na nchi mbalimbali duniani kwa ubunifu mkubwa wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotokana na Fedha za mkopo usiokuwa na riba wa Benki ya Dunia wa shilingi trilioni 1.3 kwa ajiii ya kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na changamoto ya UVIKO 19.

Aidha, aliwataka wananchi hao kutunza ipasavyo miundombinu ya mradi huo wa maji ili iweze kudumu muda mrefu na kuendelea kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Akiwa jimboni, Dkt. Nchemba ametembelea na kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya madarasa  ya shule ya Sekondari Ndulungu, kituo cha afya Mwandegembe, Shule ya Sekondari Mbelekese, Kituo cha Afya Urugu na kuzungunza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika tarafa  ya Ndago.

MWISHO