Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

UMAHIRI WA MAAFISA WAWAKOSHA VIONGOZI WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA-SABASABA

12 Jul, 2024
UMAHIRI WA MAAFISA WAWAKOSHA VIONGOZI WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA-SABASABA

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, akizungumza na Afisa Habari Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Ramadhani Kissimba (kushoto), kuhusu umuhimu wa elimu kwa umma ili kuchochea maendeleo, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

 

Viongozi mbalimbali waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, wameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuwa na mikakati mizuri ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu Majukumu na Sera za Wizara Fedha, ili kuchochea maendeleo.

Baadhi ya viongozi waliotembelea Banda ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bw. Godfred Mbanyi, Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. Fransis Mwakapalila na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha wa Wizara ya Fedha, Bi. Janeth Hiza.

Mwisho.