Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA YATETA NA UONGOZI WA IDARA YA SERA ZA KIBAJETI - IMF-FAD

17 Apr, 2024
TANZANIA YATETA NA UONGOZI WA IDARA YA SERA ZA KIBAJETI - IMF-FAD

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ameongoza Ujumbe wa Tanzania ulipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Idara ya Sera ya Kibajeti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF-FAD), Kando ya Mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kwa kutoa misaada ya kiufundi ili kuboresha mifumo na sera za kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Mcha Hassan Mcha, Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF.