Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA SITA (6) WA KAMATI MAALUM YA MAWAZIRI WA FEDHA, MIPANGO YA KIUCHUMI NA MTANGAMANO WA UMOJA WA AFRIKA.

21 Jul, 2023
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA SITA (6) WA KAMATI MAALUM YA MAWAZIRI WA FEDHA, MIPANGO YA KIUCHUMI NA MTANGAMANO WA UMOJA WA AFRIKA.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza wakati wa Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliojadili kwa pamoja masuala mbalimbali na kuweka mikakati endelevu ya kukuza uwekezaji, ukuaji jumuishi wa uchumi na ustawi wa bara la Afrika kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na majanga ya kidunia ikiwemo UVIKO-19, mgogoro baina ya Urusi na Ukraine na Mabadiliko ya Tabianchi. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya. 
 
 
Tanzania imeshiriki Mkutano wa Sita wa Kamati Maalum ya Mawaziri wa Fedha, Mipango ya kiuchumi na Mtamangano wa Afrika, uliobeba kaulimbiu ya “Afrika baada ya Majanga”: Majadiliano juu ya Uwekezaji, Ukuaji Endelevu wa Uchumi na Ustawi kwa wote”. Mkutano huo uliojumuisha nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika, umefanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.
 
Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).
 
Akizungumza baada ya mkutano huo, Mhe. Chande alisema kuwa, Mkutano huo umekua na manufaa makubwa kwa Tanzania na Bara la Afrika kwa kuwa unatoa fursa ya kujadili masuala ya msingi katika mtangamano wa Afrika ikiwemo masuala ya Kodi, Mapambano dhidi ya Fedha Haramu; uanzishwaji wa Taasisi za Fedha za Afrika, uanzishwaji wa mfumo wa kidijitali wa uangalizi wa Uwekezaji, hatua muhimu na vichocheo vya kuiwezesha Afrika kufikia malengo ya maendeleo jumuishi na endelevu.
 
“Tanzania inaungana na nchi nyingine za Umoja wa Afrika kutoa mchango wake kwenye mijadala ya agenda kwa lengo la kufikia hatua muhimu za pamoja zitazowezesha kufanyika Mageuzi ya Kimuundo, Maendeleo Endelevu na Shirikishi barani Afrika kupitia mikakati bunifu ya uwekezaji” Alisema Mhe. Chande.
 
Mhe. Chande aliongeza kuwa, katika Mkutano huo wamekubaliana kuweka kipaumbele zaidi katika Kukuza uelewa wa pamoja kuhusu mifumo ya kitaasisi na kisera inayohitajika katika kupata ufanisi kwenye jitihada za kufikia Maendeleo Endelevu na Shirikishi barani Afrika pamoja na Kuja na Azimio la Mawaziri litakaloainisha mipango ya kisera na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika ngazi ya nchi, Banda na Bara ili kufikia Maendeleo Endelevu na Shirikishi barani Afrika.
 
Aidha, Mhe. Chande ametumia jukwaa hilo kuwaalika Mawaziri hao pamoja na kuwashawishi Wakuu wao wa nchi, kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu masuala ya maendeleo ya Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Development Summit) utakaofanyika Dar es Salaam, tarehe 25 na 26 Julai 2023 chini ya uenyeji wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
 
MWISHO.