Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 6 WA WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA WA AU

18 Jul, 2023
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 6 WA WATAALAMU WA NCHI WANACHAMA WA AU
Naibu Katibu Mkuu - Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akizungumza wakati wa Mkutano wa 6 wa Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliofanyika jijini Nairobi, nchini Kenya. Kikao hicho kimelenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo.

 

Naibu Katibu Mkuu - Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 6 wa Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Kikao hicho kinafanyika tarehe 17 hadi 19 Julai 2023, katika ukumbi wa hoteli ya Movenpick, jijini Nairobi, nchini Kenya. 
 
Kikao hicho kimelenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo. 
 
Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao mbalimbali ambavyo Serikali ya Tanzania imekua ikishiriki ili kutafuta fursa mbalimbali zitakazosaidia ukuaji wa uchumi imara wa nchi.
 
MWISHO.