Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA YAJIVUNIA NAMNA ILIVYOKABILIANA NA UVIKO 19

15 Jul, 2023
TANZANIA YAJIVUNIA NAMNA ILIVYOKABILIANA NA UVIKO 19
TANZANIA imeahidi kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia makundi maalumu yakiwemo ya watu wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na athari za UVIKO 19 pamoja na kuopiga vita umasikini.
 
Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu Mwamba, wakati akichangia mjadala uliohusu namna nchi za Tanzania, Finland na Zambia zilivyoweza kukabiliana na athari za UVIKO 19 katika makundi ya kijamii ikiwemo watu wenye mahitaji maalum, kando ya Mikutano ya Jukwaa la Juu la Siasa la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.
 
Dkt. Mwamba alisema kuwa Serikali ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukabiliana na athari za UVIKO 19 kupitia mkopo usio na riba wa shilingi trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambapo miradi kadhaa ilitekelezwa katika sekta za elimu, afya, maji, utalii na kusaidia kaya masikini.
 
Alifafanua kuwa Tanzania inatekeleza mradi mkubwa wa kunusuru kaya masikini ambapo fedha zimekuwa zikitolewa na Benki ya Dunia lakini hivi sasa Serikali inaongeza Bajeti yake kila mwaka ili kuwafikia watu wengi zaidi na kuifanya program hiyo kuwa endelevu
 
Dkt. Mwamba alisema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika kipindi hicho ikiwemo uhaba wa hewa ya oksijeni, lakinji Serikali ilifanya jitihada kubwa kwa kushirikiana na Sekta Binafsi kukabiliana na hali hiyo na kushauri nchi mbalimbali kuishirikisha sekta binafsi katika kujiandaa kukabiliana na majanga kama hayo yanapojitokeza.
 
Awali akifungua Mkutano huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Balozi Hussein Kattanga, alielezea umuhimu wa nchi mbalimbali kuweka mikakati na sera madhubuti za kukabiliana na majanga kama ya UVIKO 19 ili kuwa na mipango jumuishi ya kuwaweza wananchi kiuchumi na kijamii.
 
Kwa upande wao, Wawakilishi wa nchi za Finland na Zambia, walisema kuwa nchi zao zilikabiliwa na changamoto mbalimbali za kihuduma kwa makundi yenye uhitaji maalum ikiwemo ukosefu wa miundombinu rafiki katika kipindi cha UVIKO 19.
 
Walisema kuwa licha ya changamoto hizo, ikiwemo ukosefu wa upatikanaji wa taarifa muhimu kwa makundi hayo, Serikali za nchi hizo zilifanya kila jitihada za kuboresha huduma muhimu zikiwemo za afya, elimu na maji.
 
Walitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, pamoja na sekta binafsi, kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma muhimu na kujiandaa kikamilifu wakati wa majanga kama ya UVIKO 19 ili kuiwezesha jamii hususan ya watu wenye mahitaji maalum, kuishi kwa furaha.