Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA NA DENMARK KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

08 Mar, 2023
TANZANIA NA DENMARK KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Waziri Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa Dermark imekubali kushirikiana na Tanzania katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekua yakiathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Dkt. Nchemba ameyasema hayo Doha nchini Qatar baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Sera za Mabadiliko ya Tabianchi wa Serikali ya Kifalme ya Denmark, Mhe. Dan Jorgesen, wakati wa Mkutano wa Tano wa Umoja wa  Mataifa wa nchi zinazoendelea za kipato cha chini.

Alisema nchi hizo mbili zimekubaliana kuzielekeza Taasisi zao kuendelea kushirikiana katika Nyanja mbalimbali hususani kukabiliana na mabadiliko hayo ya tabia nchi ili kukuza uchumi.

“Licha ya makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huu, tumekua na ushirikiano mzuri na Dernmark ambapo Serikali yetu hupokea fedha nyingi kupitia Taasisi za Denmark ambazo hutumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo”, alisema Dkt. Nchemba.

Alisema kuwa mkutano kati ya nchi hizo mbili ni muendelezo wa mikutano mbalimbali ambayo imekuwa ikifanyika hivyo mazungumzo ya sasa ni jitihada za kuendelea kuimarisha ushirikiano huo wa maendeleo katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Saada Mkuya, amesema kuwa Serikali ya Zanzibar imepata manufaa makubwa katika sekta za kijamii katika sekta ya  afya, elimu na miundombinu.

Alisema Zanzibar na Tanzania kwa ujumla imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha inatekeleza diplomasia ya kiuchumi na nchi mbalimbali ili kuvutia uwekezaji na kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo mikutano inayoendelea na nchi nyingine ni miongoni mwa jitihada za kufanikisha adhma hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Sera za Mabadiliko ya Tabianchi wa Serikali ya Kifalme ya Denmark, Mhe. Dan Jorgesen, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo.

Mhe.  Jorgesen amesema kuwa pamoja na upya wa Serikali yake iliyopo madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa Novemba 2022 Serikali ya mseto ya Denmark itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali.

“Mabadiliko ya Tabianchi ni masuala ambayo yanapaswa kupewa kipaumbele na kila mmoja wetu kutokana na athari zinazoendelea kujitokeza kutoka na changamoto hiyo”, alisema Mhe. Jorgesen.

Aidha, Mheshimiwa Jorgesen amesema Serikali yake inayoongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Mette Frederiksen, anao ufahamu mkubwa kuhusu siasa za Bara la Afrika hivyo itasaidia kuongeza ushirikiano kati ya Denmark na Tanzania.