Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA NA BURUNDI ZAJADILIANA UJENZI WA SGR.

18 Mar, 2024
TANZANIA NA BURUNDI ZAJADILIANA UJENZI WA SGR.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa kikao na Ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi ikiongozwa na Waziri wa Miundimbinu na Makazi, Mhe. Dieudonne Dukundane (hayupo pichani), ambapo wamejadiliana kuhusu ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) itakayounganisha nchi hizo mbili ambayo itachochea shughuli za kiuchumi. Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, kimehudhuriwa pia na Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Leontine Nzeyimana, Mkurugenzi wa Mipango na Usanifu kutoka Wizara ya Miuondombinu na Makazi Burundi, Mhandisi  Pasteur Bisekere, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Bw. Japhet Justine (wa kwanza), Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje Bw. Robert Mtengule, Kamishna Msaidizi Idara ya  Fedha za Nje Bw. James Msina na Mchumi kutoka Idara ya Fedha za Nje, Bw. Frank Mangap.
 
WAZIRI wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Miundombinu wa Burundi Mhe. Dieudonné Dukundane, kuhusu maendeleo ya Mradi wa Reli ya Kisasa SGR utakaoziunganisha nchi hizo mbili.
 
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Dodoma, Viongozi hao wamesema kuwa mradi huo utakapokamilika utachochea biashara ya madini na kilimo pamoja na kuimarisha mahusiano ya kikanda na kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.
 
Dkt. Nchemba alisema kuwa Ushirikiano wa nchi hizo mbili katika maandalizi ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) umekua mzuri na kwamba watalaamu wa pande zote mbili wameendelea na vikao hususan katika eneo la manunuzi na fedha ili kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa.
 
“Ujenzi wa Reli hii ya Kisasa ya kuunganisha nchi zetu ni muhimu sana kwetu na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa ni mradi wa Kipaumbele na anataka ukamilike” aliongeza Mhe Dkt. Nchemba
 
Alisema kuwa wataalum kutoka nchi hizo mbili wanaendelea kushirikiana ili kuhakikisha kila kitu kinafanikiwa na kufikia matarajio ya Rais wa Tanzania pamoja na Rais wa Burundi ya kuona mradi huo unafanikiwa.
 
Naye Waziri wa Miundombinu na Makazi wa Jamhuri ya Burundi, Mhe. Dieudonné Dukundane, alisema kuwa nchi yake itahakikisha kuwa mradi huo unapewa kipaumbele na tayari timu ya wataalam kutoka Burundi ipo Dar es Salaam ikiendelea kupitia masuala ya manunuzi wakishirikiana na wataalam wa Tanzania.
 
“Rais wangu Mhe. Evariste Ndayishimiye, ametuelekeza kuwa tufuatilie kwa ukaribu na kwa kipaumbele mchakato mzima unakwenda kama ilivyopangwa ili uishe vizuri, na mimi nimeishi hapa Tanzania kwa miaka sita (6) nimeona namna ambavyo SGR itakavyoharakisha maendeleo ya nchi” alisema Mhe. Dukundane.
 
Mradi huo wa Reli ya Kisasa (SGR) baada ya kukamilika hususan Ujenzi wa Reli ya Uvinza hadi Musongati nchini Burundi kutawezesha kusafirisha tani milioni 3 za madini kwa mwaka kutoka mgodi mkubwa wa madini ya Nickel uliopo Musongati nchini Burundi unaokadiriwa kuwa na hifadhi ya tani milioni 150 za madini ya Nickel, Cobalt na Copper, na pia kuimarisha shughuli za kiuchumi za nchi hizo mbili.
 
MWISHO