Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

TANZANIA KUTUMIA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MADENI (CS-MERIDIAN)

09 Aug, 2023
TANZANIA KUTUMIA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI WA MADENI (CS-MERIDIAN)

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akizungumza kabla ya kuzindua rasmi Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao Tanzania imejiunga rasmi ili kuboresha usimamizi wa taarifa za madeni, jijini Dodoma.

 

Serikali imeungana na nchi nyingine za Jumuiya ya Madola kwa kuanza kutumia Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao utaboresha upatikanaji wa taarifa za madeni.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo amesema mfumo huo utaleta tija katika kuhifadhi taarifa za madeni pamoja na kuongeza uwazi wa takwimu za madeni hayo.

“Wizara ya Fedha imeona ni muhimu kuingia kwenye mfumo mpya wa Kimataifa ambao unatumiwa na wenzetu katika Jumuiya ya Madola”, alibainisha Bi. Omolo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwandamizi wa Kurugenzi ya Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, Dkt. Ruth Kattamuri, ambaye alishiriki uzinduzi huo kwa njia ya mtandao, aliipongeza Serikali ya Tanzania kuingia katika mfumo huo na kuahidi kuwa jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ufanisi na kuleta maendeleo.

Awali akiulelezea mfumo huo, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, alisema mfumo huo ulitengenezwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa mwaka 2019.

Alisema Tanzania ilianza taratibu za kuhamia katika mfumo huo kuanzia mwezi June 2022 kwa kutumia wataalam wa ndani kutoka Bara na Zanzibar kwa kushirikiana na wataalam wa Jumuiya ya Madola na kubainisha kuwa baada ya uzinduzi huo utaanza kutumika rasmi.

Mwisho.