Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WAHALIFU

24 May, 2024
SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WAHALIFU

Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akifafanua jambo kwa baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Missenyi walioshiriki semina ya elimu ya fedha ambapo mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo utunzaji wa akiba na mikopo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.

 

Wananchi wametakiwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali kuwafichua wamiliki wa Taasisi za Ukopeshaji fedha zisizo rasmi ili watakao bainika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bw. John Wanga, alipokutana na Timu ya wataalamu ya Wizara ya Fedha ambao wanaendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa mkoa wa Kagera katika Wilaya nne za Bukoba, Missenyi, Muleba na Biharamulo.

“Sisi kama viongozi wa Serikali tunatakiwa tuendelee kushirikiana na Wananchi kuwakemea watoa huduma wasio na nia njema kwa Taifa wanaojali maslahi yao binafsi”, alisema Bw. Wanga.

Alisema kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watu wote watakaobainika kwenda kinyume na maelekezo waliyopewa na Benki Kuu ya Tanzania kabla hawajapatiwa leseni ya kuendesha shughuli za utoaji mikopo.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bw. Flavian Nturwa, alisema kuwa ni wajibu wa Waratibu wote wa Huduma Ndogo za Fedha kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi katika ngazi zote ili wawe na uelewa mpana wa masuala ya fedha.

“Tutahakikisha tunafanya mikutano ya mara kwa mara kwa wananchi wa pande zote, watoa mikopo na wapokeaji ili wawe na uelewa wa pamoja hususan elimu ya mikataba ili kuepuka kusaini mikataba yenye masharti magumu”, alisema Bw. Nturwa.

Naye mtoa Huduma za Mikopo Bw. Salehe Hamisi, alisema kuwa elimu itolewe kuhusu utaratibu wa kusajili Taasisi za Fedha ili Wafanyabiashara waweze kujisajili kwa wingi na kutambulika rasmi.

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha, Bi.Mary Mihigo, aliwasisitiza wananchi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na kutunza akiba.

Wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la utoaji elimu kwa wananchi kuhusu huduma ndogo za fedha ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na elimu ya huduma ndogo za fedha.

Mwisho.