Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YAUNDA KAMATI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA

07 Dec, 2022
SERIKALI YAUNDA KAMATI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA
SERIKALI imeunda kamati ya kutanzua mgogoro wa mipaka ya ardhi baina ya wananchi na Msitu wa Hifadhi ya Bonde la Wembere unaosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilayani Iramba mkoani Singida,  uliodumu kwa muda wa miaka mitatu.
 
Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Mary Masanja, alipotembelea eneo hilo lenye mgogoro, akiambatana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.
 
Ziara ya Mawaziri hao wawili katika Hifadhi ya Msitu wa Bonde la Wembere yenye ukubwa wa zaidi ya hekta za mraba elfu 54, unafuatia malalamiko ya wakazi wa eneo hilo ambao wamezuiwa kufanya shughuli zozote za kuwawezesha kujikimu kimaisha kwa vile wako ndani ya hifadhi.
 
Mheshimiwa Masanja alisema kuwa Serikali inataka kuona mgogoro huo unamalizika na kuitaka kamati hiyo iliyoundwakushughulikia mgogoro huo  inakamilisha kazi hiyo kwa wakati kwa kuzishirikisha kikamilifu pande zote zinazohusika ili kupata suluhu ya kudumu.
 
Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo imepewa jukumu la kupitia upya mipaka iliyowekwa na TSF na kulalamikiwa na wananchi wanaoendesha shughuli zao mbalimbali za kiuchumi katika eneo hilo zikiwemo shughuli za uvuvi, kilimo na ufugaji.
 
Aidha, Mheshimiwa Mary Masanja, aliuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika Wilaya hiyo ya Iramba, kuwarejeshea wananchi mali zao walizozikamata  na kuzishikilia ikiwemo, pikipiki na majembe ili kuendeleza hali ya utulivu na amani iliyopo katika eneo hilo.
 
Hata hivyo, Naibu Waziri huyo wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja, alikemea kitendo cha baadhi ya wananchi walioharibu miundombinu ya Mradi wa uoteshaji wa kitalu chkijiji cha Ujungu kata ya Mtekente, ikiwemo kuvunja uzio na kuharibu kisima cha maji na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 50.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alisema hatua iliychukuliwa na Serikali ya kutatua mgogoro huo kwa kuunda kamati ya kupitia upya mipaka inayolalamikiwa na wananchi imekuja wakati muafaka.
 
Alishauri kamati husika ifanyekazi hiyo kwa weledi na kwa haraka ili mgogoro huo uishe na kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao bila hofu lakini pia kuimarisha uhifadhi wa eneo hilo lenye ardhi oevu la Bonde la Wembere.
 
Aliwataka wananchi hao waendelee kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia mgogoro huo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na kwamba anatarajia mgogoro huo utamalizika lakini pia watambue umuhimu wa uwepo wa hifadhi hiyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.
 
Mgogoro wa ardhi (mipaka) baina ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na wananchi katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida unahusisha wakazi wa kata sita za Urughu, Mketenke, Mtowa, Mgongo, Ntwike, Tulya na Kadaru.
 
Mwisho