Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YATOA WITO KWA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKI MIRADI YA MAENDELEO.

15 Apr, 2026
SERIKALI YATOA WITO KWA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKI MIRADI YA MAENDELEO.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza wakati wa kikao na viongozi na wafanyakazi kutoka viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za vifungashio, madaftari na karatasi, walipomtembelea ofisini kwake, Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

 

Serikali imeendelea kuisihi sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta ya umma kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, afya na miundombinu ili kuisaidia Serikali kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe.  Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi na wafanyakazi kutoka viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za vifungashio, madaftari na karatasi, walipomtembelea ofisini kwake.

Alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unaendelea kukua na kuimarisha maisha ya Watanzania kama ilivyoelekezwa katika mpango wa maendeleo wa Taifa.

“Katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, tunalenga uchumi wa trilioni moja, ninyi ni wadau wakuu wa maendeleo ya nchi hii na tunataka ushiriki wenu uwe ni mkubwa kuliko upande wa Serikali kwa maana ya sekta ya umma’’ alisema Mhe. Mhandisi Munde.

Aliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuendelea kudhibiti uingizwaji wa bidhaa kinyume na utaratibu ili kuongeza mauzo ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya nchi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Munde aliwasisitiza wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kuendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuongeza ushindani katika soko la ndani na Kimataifa jambo litakalosaidia kuongeza mauzo.

Kwa upande wake kiongozi wa Ujumbe huo kutoka kiwanda cha vifungashio, Bw. Osman Haruni, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono na kuweka mazingira rafiki ya biashara jambo linalowahamasisha wamiliki wa viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji wa bidhaa hizo.

“Tuinashukuru Serikali inaendelea kutuunga mkono, tunaomba iendelee kutuwekea mazingira rahisi ya utekelezaji wa kazi zetu ili tuendelee kuzalisha bidhaa hizo kwa ubora zaidi” alisema Bw. Haruni.

Mwisho