Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI YASHAURIWA KUANZISHA KLINIKI YA FEDHA

16 Aug, 2024
SERIKALI YASHAURIWA KUANZISHA KLINIKI YA FEDHA
Afisa Msimamizi Mkuu wa Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bw. Salim Khalfan Kimaro, akiitambulisha Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani Lindi kutoa elimu ya fedha, kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. George Mbesigwe (katikati) na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ruangwa Bw. Rashid Namkulala.
 
Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Taasisi za kifedha ikiwemo Benki Kuu, Taasisi za Uwekezaji na Bima zimeshauriwa kuanzisha kliniki ya elimu ya fedha kipindi cha mavuno ili kuwafikia wakulima katika maeneo yao ya uzalishaji.
 
Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Bw. George Mbesigwe,  alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha ambayo ipo mkoani humo kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali wakiwemo wakulima, wafanyabiashara na  wanafunzi.
 
"Kipindi cha mavuno huku kwetu ndo kipindi ambacho wananchi wanakua na fedha, hivyo elimu hii ikitolewa wakati wa mavuno itasaidia wakulima kuhamasika kufungua akaunti benki, kufanya uwekezaji kupitia Taasisi za Uwekezaji au kukata Bima ya mazao kwakuwa zitakua zimefika katika eneo husika la mavuno" alisema Bw. Mbesigwe.
 
Aliongeza kuwa uhitaji wa elimu ya fedha kwa wananchi ni mkubwa hivyo ni vyema zoezi hilo likawa endelevu ili kuhakikisha linawafikia wananchi wengi ili waweze kupanga matumizi sahihi ya fedha zao.
 
Naye Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Edward Mbaruku, aliahidi kuendelea kuwahamasisha wananchi wa Halmashauri hiyo kujenga mazoea ya kujiwekea akiba, kukopa katika Taasisi rasmi kuepuka migogoro lakini pia kusajili vikundi ili waweze kutambulika na Serikali na kuwa na sifa yakupata mikopo na fursa nyingine zinazotolewa na Serikali kupitia vikundi.
 
Naye Afisa Msimamizi Mkuu wa Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bw. Salim Khalfan Kimaro, aliwashukuru wananchi wa Ruangwa kwa ushirikiano waliouonesha wakati wa semina kwa kuuliza maswali na kutoa ushauri ambao utazingatiwa awamu nyingine ya zoezi la utoaji elimu ya fedha.
 
 “Sisi kama Wizara ya Fedha tunaahidi kuendelea kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali ili kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na elimu hii muhimu kwa kuwa itamsaidia kupanga bajeti, kujiwekea akiba na kufanya uwekezaji na kujikwamua kiuchumi”, alisema Bw. Kimaro.
 
Katika zoezi la kutoa elimu kwa Wananchi, Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha imeambatana  na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), wakiwa mkoani Lindi watatoa elimu hiyo katika Wilaya ya Liwale, Nachingwea, Mtama, Ruangwa, Kilwa na Manispaa ya Lindi.
 
MWISHO.