Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI KUONGEZA WIGO WA KODI KWA KURASIMISHA SEKTA ISIYO RASMI

06 Sep, 2023
SERIKALI KUONGEZA WIGO WA KODI KWA KURASIMISHA SEKTA ISIYO RASMI

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (Mb), akijibu swali bungeni jijini Dodoma kwa niaba Waziri wa Fedha, kuhusu idadi ya wafanyabiashara ambao hawajaingizwa katika mfumo rasmi wa kodi na hatua zinazochukuliwa na Serikali kuwafikia.

 

Serikali inarasimisha sekta isiyo rasmi kwa kutumia kampeni ya mlango kwa mlango inayolenga kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wasiotambulika ili kupanua wigo wa kodi.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe, alibainisha hayo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, wakati akijibu swali bungeni jijini Dodoma la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Ameir Abdalla Ameir, aliyetaka kujua idadi ya wafanyabiashara ambao hawajaingizwa katika mfumo rasmi wa kodi na Serikali inachukua hatua gani kuwafikia.

Mhe. Kigahe alisema kuwa, Serikali inatenga na kujenga maeneo maalumu ya masoko kwa wafanyabiashara wadogo na kuendelea kutoa elimu na ufafanuzi wa kina kwa wananchi kuhusu masuala ya kodi ili kuhamasisha wananchi kurasimisha biashara na shughuli za kiuchumi kwa hiari.

Alisema kuwa hadi Juni 30, 2023 Mamlaka ya Mapato Tanzania ilikuwa imesajili jumla ya walipa kodi takribani milioni 4.7 sawa na asilimia 16 ya idadi ya nguvu kazi iliyopo nchini ambayo ni takribani watu milioni 33.

Alieleza kuwa idadi ndogo ya usajili wa walipakodi, ikilinganishwa na fursa ya nguvu kazi iliyopo inatokana na sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi hapa nchini kuendeshwa na sekta isiyo rasmi inayokadiriwa kuajiri takribrani watu milioni 27.7.

Mwisho.