Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI KUJENGA VITUO SITA VYA FORODHA MWAKA UJAO WA FEDHA

30 Apr, 2025
SERIKALI KUJENGA VITUO SITA VYA FORODHA MWAKA UJAO WA FEDHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Oliver Daniel Semuguruka, aliyetaka kufahamu kuhusu mpango wa Serikali wa kuanza ujenzi wa Kituo cha Forodha katika Kijiji Mukikoro Kata ya Mugoma, Wilayani Ngara, mkoani Kagera, bungeni jijini Dodoma.  

 

Serikali imesema kuwa ina mpango wa kujenga  vituo sita vya forodha mipakani katika mwaka wa fedha ujao wa 2025/26.

Hayo yalisema bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Oliver Daniel Semuguruka, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kuanza ujenzi wa Kituo cha Forodha katika Kijiji cha Mukikoro, Kata ya Mugoma - Ngara.  

Mhe. Chande alisema kuwa Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 1.1 ya ujenzi wa vituo Sita vya forodha kikiwemo kituo cha forodha Mugoma kilichopo Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Burundi kwa mwaka ujao wa fedha.

Mwisho.