Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA MPAKA WA OLAIKA

04 Nov, 2022
SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA MPAKA WA OLAIKA

Serikali imeahidi kuendelea kufuatilia mwenendo wa ukuaji wa shughuli za forodha katika mpaka wa Olaika wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, hatua itakayoiwezesha Serikali kufanya uamuzi wa kufungua Kituo cha Forodha cha kudumu katika mpaka huo.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Emmanyel Lekishon Shangai, aliyetaka kufahamu wakati ambapo Serikali itajenga Kituo cha Forodha katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Olaika ulioko Wilayani Ngorongoro.

Mhe. Chande alisema katika mwaka wa fedha 2021/22, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanya utafiti katika maeneo yote nchini yenye uhitaji wa Ofisi za kudumu za usimamizi wa kodi ukiwemo mpaka wa Olaika wilayani Ngorongoro.

“Serikali ilibaini kuwa gharama za usimamizi wa shughuli za forodha katika mpaka wa Olaika zitakuwa kubwa ikilinganishwa na kiwango cha ushuru wa forodha unaotarajiwa kukusanywa”, alibainisha Mhe. Chande.

Mwisho.