Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

PPRA NA NEEC KUONGEZA WALIPA KODI WAKUBWA

10 Feb, 2024
PPRA NA NEEC KUONGEZA WALIPA KODI WAKUBWA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, akimkabidhi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), mwongozo wa kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, wa kati na makundi maalumu katika ununuzi wa umma, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa moja ya jambo ambalo nchi inalihitaji kwa sasa ni kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, wa kati na makundi maalumu katika ununuzi wa umma ili washiriki katika shughuli za kiuchumi na kuwa walipakodi wakubwa.

Dkt. Nchemba amesema hayo jijini Dodoma wakati wa hafla ya utiaji saini wa Hati ya Makubaliano kati ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, wa kati na makundi maalumu katika ununuzi wa umma, ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, alikuwa mgeni rasmi.

“Kama kwenye nchi tutakuwa na watu hawashiriki katika shughuli za uzalishaji na Uchumi ni itakuwa vigumu sana kutengeneza walipakodi wakubwa”, alisema, Dkt. Nchemba.

Alisema wazo hilo la kuwawezesha katika ununuzi wa umma, kwa upande wa Wizara ya Fedha linaepusha kukimbizana na watu masikini kutafuta kodi hivyo kusaidia kukusanya kodi kwa watu ambao wanashiriki katika shughuli za kiuchumi na wanauwezo, jambo ambalo ni faida.

Dkt. Nchemba amemshukuru Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, kwa kukubali kushiriki katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo na kwamba baada ya zoezi hilo anaamini utekelezaji wa mawazo yaliyowekwa yatatekelezwa.

Aidha amezipongeza timu za wataalamu kwa kazi nzuri waliyofanya iliyosababisha kusainiwa kwa makubaliano hayo ambayo yataziba mapungufu yaliyokuwa yanajitokeza hususani kwenye eneo la utekelezaji kwa kuwa kuna mambo yalikuwa kwenye maandishi lakini utekelezaji ulikuwa unakosekana.

Mwisho.