Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

OMOLO ASISITIZA UANDAAJI WA MPANGO WA BAJETI WENYE TIJA.

10 Mar, 2025
OMOLO ASISITIZA UANDAAJI WA MPANGO WA BAJETI WENYE TIJA.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akifunga  Kikaokazi cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26, kikao hicho kiliwashirikisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa mikoa husika, katika Ukumbi wa Kambarage, Jijini Dodoma.
 
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, amewasisitiza Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Bajeti wa Mikoa kuandaa Mpango wa Bajeti wa Mwaka 2025/2026 wenye tija.
 
Ametoa msisitizo huo Jijini Dodoma, wakati akihitimisha kikaokazi cha siku mbili cha Uchambuzi wa Bajeti na Mipango kwa Mwaka 2025/26.
 
Kikao hicho kiliwaleta pamoja wadau wa sekta husika ili  kuainisha na kuibua maeneo ambayo mafungu yanaweza kushirikiana na kuleta ufanisi katika uandaaji na utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2025/26.
 
Uchambuzi huo unalenga kuhakikisha uratibu wa shughuli za Serikali Kisekta unaboreshwa ili kuongeza ushirikiano na nguvu ya pamoja (Synergies) katika utekelezaji wa mipango kati ya Sekta zinazotegemeana.
MWISHO.