Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MWANDUMBYA ATOA RAI KWA MAAFISA MASUULI KUBORESHA UKUSANYAJI MAPATO YASIYO YA KODI

22 Sep, 2025
MWANDUMBYA ATOA RAI KWA MAAFISA MASUULI KUBORESHA UKUSANYAJI MAPATO YASIYO YA KODI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya akiongoza Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilicholenga kujadili na kubuni mbinu za kisasa za kuboresha ukusanyaji wa Kodi, Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya ametoa rai kwa Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kuendelea kutekeleza majukumu yao ya ukusanyaji wa mapato kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo suala la uwasilishaji wa mapato ya Serikali katika Mfuko Mkuu wa Serikali kwa wakati.

Bw. Mwandumbya ametoa rai hiyo wakati wa kufunga Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma

Bw. Mwandumbya alisema kuwa wajumbe wa Kikao hicho wanatakiwa kusimamia matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki likiwemo suala la matumizi ya control number jumuishi, kufanya kazi kwa weledi bila kutumia mabavu au kukusanya ada na tozo bila kutoa huduma iliyokusudiwa.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo, kutawezesha kuondoa kero na kuweka mazingira mazuri na rafiki ya ulipaji kodi kwa hiyari baina ya walipa kodi.

Kikao hicho kililenga kujadili na kubuni mbinu za kisasa za kuboresha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya Kodi ili kuwezesha nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo bila utegemezi mkubwa kwa nchi wahisani.

Mwisho.