Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MKAGUZI MKUU WA NDANI KUONGEZA USIMAMIZI WA MAPATO NA MATUMIZI

20 Apr, 2024
MKAGUZI MKUU WA NDANI KUONGEZA USIMAMIZI WA MAPATO NA MATUMIZI

Mkaguzi Mkuu wa Ndani (IAG), Bw. Benjamini Magai (kushoto) na Msaidizi wake, Bw. Mwanyika Semroki, wakifuatilia mada za ukaguzi wa mazingira siku ya mwisho ya Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA) lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Mkaguzi Mkuu wa Ndani (IAG), Bw. Benjamini Magai amesema ofisi yake itafanya mabadiliko makubwa katika taratibu za ukaguzi katika maeneo ya mapato na matumizi kutokana na mafunzo muhimu waliyoyapata katika Mkutano wa 10 wa Shirikisho la Taasisi za Wakaguzi wa Ndani Afrika (AFIIA)

Hayo aliyasema jijini Arusha wakati wa kuhitimisha siku tano za Mkutano wa 10 wa Shirikisho hilo  uliowakutanisha zaidi ya wajumbe 1200 kutoka nchi 27 za Afrika na nje ya Afrika.

Bw. Magai alisema kuwa kutokana na kukua kwa teknolojia nchi yetu inatumia mifumo ya kielektroniki katika matumizi na ukusanyaji wa mapato, hivyo katika eneo hilo kumekuwa na vihatarishi vya udukuzi, kama nchi inatakiwa kujipanga vizuri kupitia wakaguzi wake.

“Tumejifunza mambo mengi katika mkutano huu, kuna baadhi ya maeneo inawezekana yalikuwa hayatekelezwi kwa ufanisi, kwa sasa tunakwenda kuongeza tija zaidi kwa kuwa wakaguzi wetu sasa wanaweza kufanya kaguzi za kitaalamu zaidi kuliko ilivyokuwa awali”, alisema Bw. Kigai.

Bw. Magai amesema kuwa Mkutano huo wa 10 wa Wakaguzi wa Ndani Afrika uliofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, umechochea hamasa ya kufanyakazi kwa weledi mkubwa unaoambatana na matumizi ya teknolojia ili kuhakikisha taratibu muhimu katika eneo la ukusanyaji mapato, matumizi na pia mazingira na uatawala bora zinafuatwa.

Akizungumzia kuhusu ukaguzi wa mazingira, Bw. Kigai alisema kuwa ni eneo jipya ambalo wakaguzi waliona sio muhimu lakini kwa sasa limepewa uzito mkubwa ukizingatia kwa sasa kuna athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha mafuriko, joto na maporomoko ya ardhi jambo ambalo mkaguzi anatakiwa kuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha taasisi zote za umma zinajipanga katika kukabiliana na na masuala hayo.

Aidha alisema kuwa mkutano huo ulijumuisha eneo la Utawala bora na masuala ya kitaalamu katika eneo la ukaguzi ambao ulifanyika kwa siku mbili na kufuatiwa na Kongamano lilochukua siku tatu ambalo lilijikita katika masuala ya ukaguzi wa ndani.

Alisema lengo kubwa lilikuwa kuwakutanisha wakaguzi wa ndani wa Afrika na nje ya Afrika kwa ajili ya kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali katika maeneo kadhaa yakiwemo ya ukaguzi wa hesabu, vihatarishi na mazingira.

Mwisho