Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. CHANDE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA KUDHIBITI FEDHA HARAMU NCHINI BOTSWANA

08 Sep, 2023
MHE. CHANDE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA KUDHIBITI FEDHA HARAMU NCHINI BOTSWANA

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), katikati (walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania uliohudhuria Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa  nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, unaofanyika katika hotel ya Cresta Mowana, Kasane – Botswana. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo.

 

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa  nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu (Eastern and Southern Africa Anti Money Laundering Group (ESAAMLG), unaofanyika katika mji wa Kasare, nchini Botswana, kuanzia tarehe 8 -9 Septemba, 2023.

Mkutano huo wa siku mbili, pamoja na mambo mengine, utajikita katika kujadili mifumo na mbinu mbalimbali za udhibiti wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi katika nchi wanachama wa ESAAMLG.

Aidha, Mkutano huo ambao ulitanguliwa na vikao vya Makatibu Wakuu wa nchi wanachama, ulijadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya Tathmini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, walishiriki.

Mwisho.