Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. BALOZI OMAR AKUTANA NA UJUMBE WA WIZARA YA ELIMU KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

22 Jan, 2026
MHE. BALOZI OMAR AKUTANA NA UJUMBE WA WIZARA YA ELIMU KUJADILI MIKAKATI YA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (wa tatu kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha kujadili masuala mbalimbali kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu nchini, katika ukumbi wa mikutano wa Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

 

Waziri wa Fedha, Mhe.Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo Ujumbe kutoka Wizara ya Elimu Sayansi Na Teknolojia ikiongozwa na, Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo mazungumzo yao yakijikita kujadili mafanikio na changaoto za sekta ya elimu nchini, pamoja na kupanga mikakati ya kuboresha zaidi sekta hiyo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa juu wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Elimu wakimemo Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Wizara hizo.

MWISHO