Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. BALOZI OMAR AKAGUA JENGO JIPYA LA KISASA LA OFISI YA WIZARA YA FEDHA

17 Jan, 2026
MHE. BALOZI OMAR AKAGUA JENGO JIPYA LA KISASA LA OFISI YA WIZARA YA FEDHA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (mwenye shati ya batiki), akisikiliza maelezo ya namna ya kutumia mifumo ya usalama na utambuzi iliyopo katika Jengo jipya la Wizara ya Fedha lililopo katika Mji wa Serikali-Mtumba, jijini Dodoma, kutoka kwa Afisa Tehama wa Wizara hiyo, Bw. Boniface Munishi (kulia), wakati alipotembelea Kukagua Jengo hilo la Ofisi la kisasa lenye ghorofa 11, akiambatana na Naibu Mawaziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mhe. Laurent Luswetula (Mb) pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Fedha ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Jengo jipya la kisasa la Ofisi za Wizara ya Fedha lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma, litawawezesha watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi katika mazingira bora na kuwahudumia wananchi na wadau wake wengine kwa ufanisi zaidi.

Mhe. Balozi Omar, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo hilo akiambatana na Naibu Mawaziri wake wawili, Mhe. Larent Luswetula, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, na Menejimenti ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba.

Aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwezesha jengo hilo kujengwa na kukamilika.

Mhe. Balozi Omar, aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kulitunza Jengo hilo na kuhakikisha kuwa mifumo yake ya ulinzi na usalama inasimamiwa ipasavyo.

Wakizungumza katika ziara hiyo, Naibu Mawaziri, Mhe. Laurent Luswetula (Mb) na Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), walisema kuwa Jengo hilo ni la kisasa na limejengwa kwa viwango vya hali ya juu.

Akitoa taarifa wa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo kutoka Wizara ya Fedha, Mhandisi Japhet Mkwamira, alisema kuwa ujenzi wa Jengo lenye ghorofa 11 ambalo ni Jengo refu kuliko majengo yote ya Serikali yaliyopo Mji wa Serikali-Mtumba kwa sasa, limekamilika kwa asilimia 98.

Jengo hilo la Wizara ya Fedha, linajengwa na Mkandarasi Mkuu Kampuni ya Estim Construcion Co. Ltd, na Mshauri Elekezi wa mradi, ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likishirikiana na IPA Architects Ltd katika Usanifu na Usimamizi wa ujenzi,

Mwisho