Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

MHE. BALOZI OMAR AKABIDHI TUZO ZA UBUNIFU ZA TRA

27 Feb, 2026
MHE. BALOZI OMAR AKABIDHI TUZO ZA UBUNIFU ZA TRA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekabidhi tuzo za fedha taslim, ngao na vyeti kwa washindi 9 waliowasilisha mawazo bora ya ubunifu yatayosaidia katika kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Serikali na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), zenye thamani ya shilingi milioni 240, zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, baada ya kushindanisha mawazo bunifu 5,681 yaliyowasilishwa na wananchi pamoja na watumishi wa TRA, kuanzia mwezi Mei, 2025.

Mawazo Bunifu hayo yanahusisha ubunifu wa Mifumo ya Tehama ambayo imebuniwa na vijana wa kitanzania inayotarajiwa kutumiwa na TRA kuboresha wigo wa walipa kodi, kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiforodha na ulipaji kodi kwa njia rahisi na yenye ufanisi kutoka kwa walipakodi.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, aliwataja washindi hao kuwa ni Gabriel Mashenene, Edmund Komba, Emma Sambaya, Malehe Masubi, Ng’wang’wa Loyani, Erick Joachim, Ajra Noordin Ismail, Hubayb Said, na Ismail Mkumbi.

Aliwapongeza vijana hao waliotwaa tuzo hizo kwa kuwasilisha Mawazo yao ya ubunifu yatakayochangia kuimarisha utendajikazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na pia kuongeza wigo wa utoaji huduma na ukusanyaji kodi za Serikali ambazo zinatumika kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, aliimwagia sifa TRA kwa kuja na wazo hilo la ubunifu la kuongeza ukusanyaji maoni ya wananchi wengi zaidi kuhusu namna ya kuongeza ufanisi wa ukusanyaji kodi, kuliko utaratibu wa kawaida wa kutafuta namna ya kuongeza wigo wa walipa kodi na vyanzo vya mapato kwa kutumia mfumo wa ndani ya Serikali pekee.

Mhe. Balozi Omar alisema kuwa anaamini watu wengi zaidi watajitokeza kushiriki katika shindano lijalo la uwasilishaji wa mawazo hayo bunifu kutokana na manufaa waliyoyapa vijana hao tisa ambapo mshindi wa kwanza amezawadiwa shilingi milioni 50, washindi watatu wa kundi la pili wamezawadiwa shilingi milioni 30 kila mmoja na washindi watano wa daraja la tatu wamezawadiwa shilingi milioni 20 kila mmoja.

MWISHO