Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

KATIBU MKUU HAZINA ATETA NA BALOZI WA DENMARK NCHINI TANZANIA

28 Apr, 2023
KATIBU MKUU HAZINA ATETA NA BALOZI WA DENMARK NCHINI TANZANIA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamary Mwamba (katikati), Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Norgaard Dissingspandet, (kushoto), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yao katika Ofisi za Hazina Ndogo Jijini Dar es Salaam, ambapo Denmark imeahidi kuendelea kuipa ushirikiano Tanzania kwa kutoa fedha katika sekta ya afya na kuchangia Bajeti ya Serikali

 

Denmark imeahidi kuendeleza ushirikiano zaidi na Tanzania katika jitihada zake za kuimarisha uchumi na maendeleo ya wananchi kwa kutoa fedha na misaada ya kiufundi katika sekta ya mbalimbali ikiwemo afya.

Ahadi hiyo imetolewa na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Norgaard Dissingspandet alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-Maamary Mwamba, katika Ofisi Ndogo za Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.

“Denmark imekuwa ikishirikiana na Tanzania kwa miaka mingi kwa kusaidia utekelezaji wa bajeti ya Serikali, kusaidia ujenzi wa mifumo ya udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali, kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi na masuala ya afya kupitia ubia wa sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwenye Asasi zisizo za Kiserikali (AZAKI) ambapo ushirikiano huo umeleta matokeo chanya kwenye sekta hiyo” alisema Mhe. Mette

Mhe. Mette amepongeza juhudi zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusimamia maendeleo na kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya watu kwajumla.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamary Mwamba ameishukuru Denmark kwa ushirikiano na mchango wao mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea  pia kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma nzuri katika sekta ya afya na kutumia fursa za ushirikiano wa nchi hizo mbili kuwahudumia Watanzania.

Ushirikiano wa Tanzania na Denmark umetimiza zaidi ya miaka 60 na kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuanzisha ushirikiano na Serikali ya Denmark ikiwa ni baada ya mwaka mmoja tu tangu Bunge la nchi hiyo kupitisha sheria ya Ushirikiano wa Kimataifa mwaka 1962.

MWISHO