Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

HATUA YETU NI KUBWA

12 Jun, 2025
HATUA YETU NI KUBWA

HATUA YETU NI KUBWA

 

1. Imeshasomwa Bajeti,

Kwa mwaka ujao kati,

Ni kazi kujizatiti,

Hatua yetu ni kubwa.

 

2. Hii Awamu ya Sita,

Mwishomwisho tunapeta,

Ni mengi tumeyapata,

Hatua yetu ni kubwa.

 

3. Serikali ya Samia,

Hapa twaiangalia,

Pale ilipofikia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

4. Sekta zetu mtambuka,

Ni mengi yamefanyika,

Pazuri tumeshafika,

Hatua yetu ni kubwa.

 

5. Baadhi kazisemea,

Waziri kaelezea,

Vema tumezipokea,

Hatua yetu ni kubwa.

 

6. Mwaka ujao wa fedha,

Bajeti inayo ladha,

Kuondoa ya bughudha,

Hatua yetu ni kubwa.

 

7. Ni hatua kwa hatua,

Bajeti twaichambua,

Ni vema kiti chukua,

Hatua yetu ni kubwa.

 

8. Miundombinu ya afya,

Wataalam wa afya,

Hata huduma za afya,

Hatua yetu ni kubwa.

 

9. Mambo ya umaskini,

Umepungua nchini,

Anayebisha ni nani,

Hatua yetu ni kubwa.

 

10. Misukosuko dunia,

Ambayo imetujia,

Vema tumepambania,

Hatua yetu ni kubwa.

 

11. Kwetu kaya maskini,

Zilizokuwa nchini,

Wamepewa vya thamani,

Hatua yetu ni kubwa.

 

12. Kwa upande wa elimu,

Maendeleo yadumu,

Kwa kukuza ufahamu,

Hatua yetu ni kubwa.

 

13. Kwa ruzuku ya mbolea,

Dola imejitolea,

Kilimo twachekelea,

Hatua yetu ni kubwa.

 

14. UVIKO ilitikisa,

KIla mtu limgusa,

Na vita Ukraine hasa,

Hatua yetu ni kubwa.

 

15. Uhaba dola dunia,

Nchi nyingi zililia,

Tumeweza Tanzania,

Hatua yetu ni kubwa.

 

16. Hatua tulichukua,

Sekta tukakagua,

Pengo tukalitambua,

Hatua yetu ni kubwa.

 

17. Bidhaa kutoka nje,

Ya kwamba sasa zisije,

Tunajua tufanyeje,

Hatua yetu ni kubwa.

 

18. Viwanda vyetu vya ndani,

Kuongezea thamani,

Vitazalishwa nchini,

Hatua yetu ni kubwa.

 

19. Misingi amani yetu,

Ya pekee hapa kwetu,

Hiyo hasa tunu kwetu,

Hatua yetu ni kubwa.

 

20. Tuache kuichezea,

Amani ikapepea,

Ulinzi kuendelea,

Hatua yetu ni kubwa.

 

21. Tutunze yetu amani,

HIyo kwetu ya thamani,

Vurugu tusitamani,

Hatua yetu ni kubwa.

 

22. Kwa kila Mtanzania,

Ni vema awe na nia,

Amani kutulindia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

23. Hapa vyombo vya ulinzi,

Havikutaka upuzi,

Kwao hasa kazikazi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

24. Wala tusijesahau,

Amani tukadharau,

Tuna raha angalau,

Hatua yetu ni kubwa.

 

25. Vyombo vyetu vya ulinzi,

Na usalama ni kazi,

Zidi fanya kwa ujuzi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

26. Asiwepo hata mtu,

Kudharau vyombo vyetu,

Ndio usalama wetu,

Hatua yetu ni kubwa.

 

27. Uchochezi wa adui,

Asidhani hatujui,

Mali zetu hachukui,

Hatua yetu ni kubwa.

 

28. Uchochezi hutokea,

Chaguzi kuelekea,

Hili lipate elea,

Hatua yetu ni kubwa.

 

29. Ni vema tuwe makini,

Nchi yetu tuthamini,

Na tuilinde amani,

Hatua yetu ni kubwa.

 

30. Yashiriki Tanzania,

Amani kutulindia,

Afrika na dunia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

31. Bajeti ya mwaka huu,

Inayo mambo makuu,

Uchumi mekuwa juu,

Hatia yetu ni kubwa.

 

32. Miradi kimkakati,

Ilikuwa katikati,

Sasa tuko madhubuti,

Hatua yetu ni kubwa.

 

33. Kwa mradi wa umeme,

Hizi alama tusome,

Umeisha usipime,

Hatua yetu ni kubwa.

 

34. Kule Kigongo Busisi,

Ni daraja liko nasi,

Hakuna wa kutughasi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

35. Mradi ya SGR,

Maendeleo ni bora,

Dar-Dom ni ishara,

Hatua yetu ni kubwa.

 

36. Sasa wengi abiria,

Usafiri watumia,

Dar-Dom kufikia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

37. Kutoka masaa nane,

Yamepungua manne,

Kasi kubwa uione,

Hatua yetu ni kubwa.

 

38. Reli kujengwa yazidi,

Kutimiza akidi,

Kwa hatua makusudi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

39. Kwenye viwanja vya ndege,

Kuna lami hata zege,

Vingi vyajengwa vya ndege,

Hatua yetu ni kubwa.

 

40. Hata idadi ya ndege,

Mbele tuache tusonge,

Hivi ni nani apinge,

Hatua yetu ni kubwa.

 

41. Madaraja yamejengwa,

Barabara zinajengwa,

Fedha nyingi zinatengwa,

Hatua yetu ni kubwa.

 

42. Barabara nyingi mpya,

Ujenzi unaogofya,

Ni nyingi kwa yetu afya,

Hatua yetu ni kubwa.

 

43. Ujenzi Bomba mafuta,

Mikoa mingi lapita,

Hadi Tanga kuipata,

Hatua yetu ni kubwa.

 

44. Hili tuko na Uganda,

Mafuta ghafi kupanda,

Tanga kutoka Uganda,

Hatua yetu ni kubwa.

 

45. Na hii nishati safi,

Kuni mkaa ni ghafi,

Maisha nishati safi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

46. Na kwa vituo vya afya,

Watu wakipigiga chafya,

Tuweze kujenga afya,

Hatua yetu ni kubwa.

 

47. Sipitali zimejengwa,

Na vituo vimejengwa,

Watalamu wanapangwa,

Hatua yetu ni kubwa.

 

48. Ukipenda afya yako,

Kwa maendeleo yako,

Haya yote mema kwako,

Hatua yetu ni kubwa.

 

49. Afya mama na mtoto,

Zaongezeka mvuto,

Huduma si za kitoto,

Hatua yetu ni kubwa.

 

50. Bima ya afya kwa wote,

Hii iache ipite,

Ili tufaidi wote,

Hatua yetu ni kubwa.

 

51. Mipango kikamilika,

Bima ya afya kufika,

Hapo sote tutacheka,

Hatua yetu ni kubwa.

 

52. Kwa upande wa elimu,

Maendeleo yadumu,

Madarasa ya kudumu,

Hatua yetu ni kubwa.

 

53. Kwa vyumba vya madarasa,

Vimeongezeka hasa,

Kwa elimu ni hamasa,

Hatua yetu ni kubwa.

 

54. Elimu kugharamia,

Ni pekee Tanzania,

Wengi tunafurahia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

55. Udahili wanafunzi,

Ufundi kwa wanafunzi,

Tunazidi panda ngazi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

56. HUduma zile za maji,

Miradi ile ya maji,

Ambayo twaihitaji,

Hatua yetu ni kubwa.

 

57. Mradi wa kule Same,

Ulikwama usipime,

Sasa takwimu zisome,

Hatua yetu ni kubwa.

 

58. Hapo wananchi wengi,

Maji huduma msingi,

Wanapata hayo mengi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

59. Watu kuwatua ndoo,

Mama Samia jogoo,

Kama ni magoli goo,

Hatua yetu ni kubwa.

 

60. Umeme hapa nchini,

Ni kama tuko enzini,

Livyosambaa nchini,

Hatua yetu ni kubwa.

 

61. Ni vijiji kwa vijiji,

Ni kazi siyo kipaji,

Wengi unatufariji,

Hatua yetu ni kubwa.

 

62. Sasa viwanda vidogo,

Kama kuchanja magogo,

Na kuchakata mifugo,

Hatua yetu ni kubwa.

 

63. Kukimbilia mjini,

Kwa giza la vijijini,

Sasa jambo la zamani,

Hatua yetu ni kubwa.

 

64. Si kirahisirahisi,

Serikali ya Rais,

Hii REA kuwa nasi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

65. Twende na vitongojini,

Vyote vitoke gizani,

Sote tuishi nuruni,

Hatua yetu ni kubwa.

 

66. Yale yalishindikana,

Kutatua tunaona,

Kukwamakwama hakuna, 

Hatua yetu ni kubwa.

 

67. Matarajio tunayo,

Bajeti iwe ni ndiyo,

Siyo kupiga miayo,

Hatua yetu ni kubwa.

 

68. Mbele tukiendelea,

Tuzidi kuchelea,

Yetu yasijepelea,

Hatua yetu ni kubwa.

 

69. Heri tunaitakia,

Nchi yetu Tanzania,

Ngazi zidi jipandia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

70. Nawe wa fedha Waziri,

Kazi yako leo nzuri,

Twajionea fahari,

Hatua yetu ni kubwa.

 

71. Na Rais wetu pia,

Umeshaweza Samia,

Kuongoza Tanzania,

Hatua yetu ni kubwa.

 

72. Mbele kwa hizi chaguzi,

Heri wote viongozi,

Wawania uchaguzi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

73. Kile tunakitakia,

Hapa kwetu Tanzania,

Wala tusijesinzia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

74. Iwe katika uchumi,

Tuhakiki hatukwami,

Tuendelee kitemi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

75. Kwa hivi vyanzo vya fedha,

Tulipe tupate ladha,

Tena pasi na bughudha,

Hatua yetu ni kubwa.

 

76. Kwenye usafirishaji,

Iongezeke mitaji,

Na hata wawekezaji,

Hatua yetu ni kubwa.

 

77. Hata katika viwanda,

Ujenzi uweze panda,

Tupate tunavyopenda,

Hatua yetu ni kubwa.

 

78. Vitu nje kuagiza,

Idadi tukipunguza,

Tazidi kujipongeza,

Hatua yetu ni kubwa.

 

79. Shilingi kuitumia,

Bidhaa kununulia,

Na hata huduma pia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

80. Na pia kwa sekta zote,

Maendeleo tupate,

Kwamba tuzidi tupete,

Hatua yetu ni kubwa.

 

81. Sekta ya uwindaji,

Na utalii mtaji,

Sana tunazihitaji,

Hatua yetu ni kubwa.

 

Na kwao wafanyakazi,

Vema wapandishwe ngazi,

Jinsi wanachapa kazi,

Hatua yetu ni kubwa.

 

Ruzuku kwenye kilimo,

Tukuze sana kilimo,

Na manufaa yawemo,

Hatua yetu ni kubwa.

 

82. Kubwa la kuliombea,

Na hata kulitetea,

Amani kuendelea,

Hatua yetu ni kubwa.

 

83. Heri tunaitakia,

Nchi yetu Tanzania,

Tuweze kufurahia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

84. Bajeti kutekeleza,

Yote tunayoyaweza,

Tuzidi kujiongeza,

Hatua yetu ni kubwa.

 

85. Bunge muda waishia,

Kazi mmetufanyia,

Heri tunawatakia,

Hatua yetu ni kubwa.

 

Na Lwaga Mwambande (KiMPAB)

lwagha@gmail.com 0767223602