Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

FEDHA ZA UVIKO -19 KIASI CHA SH. TRIL 1.29 ZILIBORESHA SEKTA TANO

06 Feb, 2024
FEDHA ZA UVIKO -19 KIASI CHA SH. TRIL 1.29 ZILIBORESHA SEKTA TANO

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalaum, Mhe. Nusrat Shaaban Hanje, kuhusu miradi iliyotekelezwa kwa fedha za Uviko – 19 na swali la Mbunge Viti Maalum, Mhe. Janejelly Ntate, kuhusu changamoto ya uhaba wa watumishi katika vyombo vya Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) na Baraza la Rufani za Kodi (TRAT).

 

Serikali imetumia fedha za UVIKO-19 kiasi cha shilingi trilioni 1.29 zilizotolewa kama mkopo nafuu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kutekeleza mirandi katika sekta za maji, elimu, utalii, afya na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalaum, Mhe. Nusrat Shaaban Hanje, aliyetaka kufahamu miradi iliyotekelezwa kwa fedha za Uviko – 19

Mhe. Chande alisema kuwa katika Sekta ya Majifedha za mkopo zilitumika kununua mitambo 25 ya kuchimba visima, seti tano za mitambo ya kuchimba na kujenga mabwawa, seti nne za vifaa vya uchunguzi wa maji chini ya ardhi na miradi ya maji 172 vijijini na miradi 46 mijini.

Alisema Sekta ya elimu yalijengwa madarasa 12,000 (shule za sekondari) na 3,000 (shule za msingi shikizi), ukamilishaji wa vyuo vinne vya VETA ngazi ya mikoa na vyuo 25 ngazi ya wilaya na ununuzi wa vifaa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwenye vyuo 11 vya elimu ya juu.

Sekta zingine zilizotumia mkopo wa Uviko – 19 ni pamoja na Sekta ya Utalii ambapo mitambo mitano (5) ilinunuliwa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwenye hifadhi 13 za Taifa na kuimarisha mifumo ya utangazaji wa fursa za utalii ikiwemo The Royal Tour.

Kwa upande wa sekta ya Sekta ya Afya, Mhe. Chande alisema miradi iliyotekelezwa ni ujenzi na ukarabati wa vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali 70 na miundombinu ya kutolea Huduma za Dharura (EMD) katika hospitali 101, ununuzi wa X-ray 169, CT-Scan 29, MRI nne na mashine za huduma za uchunguzi wa moyo -Echo Cardiography 7  na ujenzi wa nyumba 150 za wafanyakazi.

“Fedha za mkopo zilitumika katika uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ambapo Serikali imeboresha miundombinu na mazingira ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara wadogo (wamachinga) eneo la Bahi Road Dodoma, Halmashauri za Majiji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Tanga, Mbeya, Morogoro pamoja na Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni, Temeke na  Ubungo mkoani Dar es Salaam” Aliongeza Mhe. Chande

Naibu Waziri Mhe. Chande alisema  shilingi bilioni 5.542 zimetumika kusaidia kaya maskini 51,290 zilizotambuliwa katika halmashauri 35 kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).

Kwa upande mwingine akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Mhe. Janejelly Ntate aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itamaliza changamoto ya uhaba wa watumishi katika vyombo vya Baraza la Rufani za Kodi (TRAT) na Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB), Mhe. Chande alisema kuwa TRAB ina jumla ya watumishi 27, ambao kwa sehemu kubwa wanamudu kutekeleza majukumu ya taasisi ikilinganishwa na ikama ya watumishi 35

Aidha alieleza kuwa kwa upande wa TRAT inapaswa kuwa na watumishi 36, ambapo kwa sasa kuna watumishi 15, hivyo Wizara ya Fedha imefanya “head hunting ya kupata watumishi wanne wenye uzoefu na kuwasilisha maombi ya uhamisho Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mwezi Januari, 2024 ili kutatua changamoto hiyo.

Mwisho.