Category Title
-
18 Feb, 2023THE ANTI-MONEY LAUNDERING ACT , CAP 423, R.E 2022
-
18 Feb, 2023THE ANTI-MONEY LAUNDERING ACT, CAP 423 R.E. 2022.
-
18 Feb, 2023THE ELECTRONIC TRANSACTIONS ACT, CAP 442 R.E. 2022
-
18 Feb, 2023THE_FINANCE_ACT_2022
-
17 Feb, 2023FINANCE ACT- 2021 - Amendment of Government Loans, Guarantees and Grant, Act
-
16 Feb, 2023CHAPTER 439-THE BUDGET ACT.doc FINAL REVISED 2020
-
16 Feb, 2023CHAPTER_290-THE_LOCAL_GOVERNMENT_FINANCE_ACT-01
-
16 Feb, 2023PUBLIC FINANCE ACT, CAP 348 RE 2020
-
16 Feb, 2023THE ANTI-MONEY LAUNDERING ACT, CAP 423 R.E. 2019
-
16 Feb, 2023THE BANKRUPTCY ACT, CAP 25 R.E 2019
-
View All
-
19 Jun, 2024THE PUBLIC FINANCE (MANAGEMENT OF PUBLIC PROPERTY) REGULATIONS, 2024
-
17 Feb, 2023KANUNI ZA MSAMAHA WA RIBA YA MALIMBIKIZO YA KODI YA PANGO LA ARDHI ZA MWAKA 2022
-
17 Feb, 2023THE-PUBLIC-FINANCE-GOVERNMENT-e-PAYMENT-GATEWAY-REGULATIONS-2019
-
16 Feb, 2023AMLA Regulations, June 2022 (GN 397)
-
16 Feb, 2023GN No 121-Public Procurement (Amendment) Regulations April ,2016
-
16 Feb, 2023GN.68 OF 2008- Government loans Regulations
-
16 Feb, 2023KANUNI ZA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA (VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA VYA KIJAMII) LA MWAKA 2019
-
16 Feb, 2023KANUNI ZA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA (WATOA HUDUMA NDOGO WASIOPOKEA AMANA) LA MWAKA 2019
-
16 Feb, 2023KANUNI ZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA TOZO YA MIAMALA YA FEDHA YA KIELETRONIKI ZA MWAKA 2022
-
16 Feb, 2023Public Procurement Ammendment_Act_2016
-
View All
-
10 Dec, 2024MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2025.26
-
12 Feb, 2024PLAN AND BUDGET GUIDELINE FOR 2024/25
-
17 Nov, 2023MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2024_25
-
08 Sep, 2023GUIDELINES FOR RISK MANAGEMENT IN PSE, 2023
-
08 Sep, 2023GUIDELINES FOR FRAUD RISK MANAGEMENT FRAMEWORK IN THE PUBLIC SECTOR ENTITIES, 2023
-
12 May, 2023Compensation Claims Settlement Guidelines 2023
-
02 Dec, 2022MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2023/24
-
28 Feb, 2022MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2022/23
-
28 Feb, 2022MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2021/22
-
13 Nov, 2021Guidelines For Preparation of Plans and Budget 2020_21
-
View All
-
03 Jan, 2025Midterm Review MoF Strategic Plan Final 2025-26.
-
24 May, 2024ENVIRONMENTAL AND SOCIAL COMMITMENT PLAN (ESCP) FAST PROJECT
-
24 May, 2024FINANCIAL ACCESS FOR SUSTAINABLE AND TRANSFORMATIONAL (FAST) GROWTH
-
28 Jul, 2023MPANGO WA TAIFA WA MAENDELEO 2023/2024
-
11 Jul, 2023Tanzania’s 2023 Voluntary National Review (VNR) Report on the Implementation of the 2030 Agenda for Sustainable Development
-
10 Jul, 2023Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2021.22
-
17 Jan, 2023Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi na Programu za Maendeleo
-
21 Dec, 2022MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2023-24 (2) (1) (1)
-
19 Dec, 2022REVISED STRATEGY FOR MANAGEMENT OF ARREARS
-
29 Nov, 2022PFMRP VI STRATEGY
-
View All
-
Government Budget Speeches
-
Ministry's Budget Speeches
-
12 Jun, 2025HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI 2025/2026
-
12 Jun, 2025FISCAL RISKS STATEMENT
-
17 Feb, 2023SPEECH OF GOVERNMENT BUDGET FOR 2022-23
-
14 Jun, 2022BUDGET SPEECH 2022-23 ENGLISH VERSION
-
08 May, 2022SPEECH OF GOVERNMENT BUDGET FOR 2021-22
-
08 May, 2022HOTUBA YA BAJETI KUU MWAKA 2021-22
-
08 May, 2022HOTUBA YA BAJETI KUU MWAKA 2021-22
-
07 May, 2022SPEECH OF GOVERNMENT BUDGET FOR 2020-21
-
07 May, 2022HOTUBA YA BAJETI KUU MWAKA 2020-21
-
06 May, 2022SPEECH OF GOVERNMENT BUDGET FOR 2019-20
-
View All
-
07 Jun, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2023-24
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2022-2023
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2021 - 2022
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2020 - 2021
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2016 - 2017
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2015 - 2016
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2014- 2015
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2006 - 2007
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadio ya Mapato na matumizi 2018-2019
-
17 Feb, 2023Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadio ya Mapato na matumizi 2017-2018
-
View All
-
25 Jun, 2025BUDGET EXECUTION REPORT FOR THE THIRD QUARTER OF 2024/25 (JANUARY – MARCH 2025)
-
24 Mar, 2025THE BUDGET EXECUTION REPORT FOR THE SECOND QUARTER OF 2024/25 (JULY TO DECEMBER 2024)
-
27 Dec, 2024THE BUDGET EXECUTION REPORT FOR THE FIRST QUARTER OF THE YEAR 2024/25
-
08 Nov, 2024BUDGET EXECUTION REPORT FOR THE FOURTH QUARTER_2023-24
-
31 May, 2024BUDGET EXECUTION REPORT QUATER 3- 2023-24
-
03 Apr, 2024BUDGET EXECUTION REPORT SECOND QUARTER FOR 2023_24
-
23 Jan, 2024BUDGET EXECUTION REPORT Q1 2023-24
-
28 Nov, 2023BUDGET EXECUTION REPORT FOR 2022_23 (JULY 2022 TO JUNE 2023)
-
31 May, 2023THE BUDGET EXECUTION REPORT FOR THE THIRD QUARTER OF 2022/23 (JULY 2022 TO MARCH 2023)
-
11 Apr, 2023THE BUDGET EXECUTION REPORT FOR THE SECOND QUARTER OF 2022/23
-
View All
-
14 Nov, 2024KITABU CHA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2024_25 TOLEO LA MWANANCHI
-
10 Oct, 2023GOVERNMENT BUDGET CITIZENS’ EDITION 2023/2024
-
04 Aug, 2023KEY POINTS OF TAX POLICIES IN THE 2023/24 BUDGET SPEECH - CITIZEN EDITION
-
26 Jul, 2023BUDGET INSIGHTS 2023_24
-
16 Aug, 2022Citizen Budget 2022_23 English
-
03 Mar, 2022GOVERNMENT BUDGET CITIZENS’ EDITION 2021/2022
-
02 Mar, 2022GOVERNMENT BUDGET CITIZENS’ EDITION 2020/2021
-
01 Mar, 2022GOVERNMENT BUDGET CITIZENS’ EDITION 2019/2020
-
28 Feb, 2022GOVERNMENT BUDGET CITIZENS’ EDITION 2018/2019
-
25 Feb, 2022GOVERNMENT BUDGET CITIZENS’ EDITION 2017/2018
-
View All
-
Budget Books 2024/2025
-
Budget Books 2023/2024
-
Budget Books 2022/2023
-
Budget Books 2021/2022
-
Budget Books 2020
-
Budget Books 2018/2019
-
Budget Books 2015/2016
-
Budget Books 2014/2015
-
23 Oct, 2024volume I 2024-25 as passed by Parliament
-
26 Aug, 2024Vol II Recurent Expenditure As Passed 202425
-
26 Aug, 2024Vol III Recurrent Expenditure As Passed 202425
-
26 Aug, 2024Vol IV Development Expenditure As Passed 2024_25-2
-
03 May, 2024Vol I Revenue Estimates as Submitted 2024.25
-
19 Apr, 2024Vol II Reccurent Expenditure As Submitted 2024.25
-
19 Apr, 2024Vol III Recurrent Expenditure As Submitted 2024.25
-
19 Apr, 2024Vol IV Development Expenditure As Submitted 2024.25
-
View All
-
02 May, 2025Volume II As Submitted 2025.26
-
02 May, 2025Volume III As Submitted 2025.26
-
02 May, 2025Volume IV As Submitted 2025.26
-
28 Aug, 2023Vol II Recurrent Expenditure As Passed 2023.24
-
28 Aug, 2023Vol III Recurrent Expenditure As Passed 2023.24
-
28 Aug, 2023Vol IV Development Expenditure As Passed 2023.24
-
04 Apr, 2023VOL II Recurrent Expenditure As Submitted 2023-24
-
04 Apr, 2023VOL III Recurrent Expenditure As Submitted 2023-24
-
04 Apr, 2023VOL IV Development Expenditure As Submitted 2023.24
-
View All
-
07 Nov, 2022VOLUME I REVENUE_ESTIMATES_2022_23 AS PASSED BY THE PARLIAMENT
-
10 Oct, 2022As Passed Volume II 2022_23
-
10 Oct, 2022As Passed Volume III 2022_23
-
10 Oct, 2022As passed Volume IV 2022_23
-
19 Jul, 2022Revenue_estimates_22_23
-
07 Jun, 2022VOLUME II As Submitted 2022_23
-
07 Jun, 2022VOLUME III As Submitted 2022_23
-
07 Jun, 2022VOLUME IV As Submitted 2022_23
-
View All
-
29 Jun, 2022VOLUME IV AS PASSED BY PARLIAMENT 2021.22
-
01 Jun, 2022VOLUME II AS PASSED BY PARLIAMENT 2021.22
-
31 May, 2022VOLUME III AS PASSED BY PARLIAMENT 2021.22
-
07 Mar, 2022VOLUME II ESTIMATES OF PUBLIC EXPENDITURES AS PASSED BY THE PARLIAMENT 2021.2022 (MINISTERIAL)
-
06 Mar, 2022VOLUME III ESTIMATES OF PUBLIC EXPENDITURES AS PASSED BY THE PARLIAMENT 2021.2022 (REGIONAL)
-
05 Mar, 2022VOLUME IV PUBLIC EXPENDITURE ESTIMATES DEVELOPMENT VOTES AS PASSED BY THE PARLIAMENT 2021.2022 (Ministerial and Regional Development Programmes)
-
04 Mar, 2022VOLUME I Financial Statement & Revenue Estimates for the year from 1 July 2021- to 30th June 2022
-
03 Mar, 2022VOLUME II Estimates of Public Expenditure Consolidated Fund Services and Supply Votes (Ministerial) - 2021.22
-
28 Feb, 2022VOLUME III Estimates of Public Expenditure Supply Votes (Regional) - 2021-22
-
27 Feb, 2022VOLUME IV Public Expenditure Estimates Development Votes (Ministerial and Regional Development Programmes ) - 2021.22
-
View All
- Content not found
-
03 Mar, 2022VOLUME I - FINANCIAL STATEMENT AND REVENUE ESTIMATES 2018-19
-
02 Mar, 2022volome II 2018_19
-
28 Feb, 2022Volume III 2018_19
-
27 Feb, 2022volome IV 2018_19
-
26 Feb, 2022KITABU CHA MKAKATI WA KUZIWEZESHA HALMASHAURI KUJITEGEMEA KIMAPATO
-
View All
-
03 Mar, 2022Volume II -as passed 2014-15
-
02 Mar, 2022Volume III -as passed 2014-15
-
01 Mar, 2022volume IV-as passed 2014-15
-
View All
- Content not found
- Content not found
-
13 Mar, 2023MAPENDEKEZO YA SERIKALI YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2023/24 NA MFUMO NA UKOMO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2023/24
-
17 Feb, 2023HOTUBA YA HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2021 NA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2022-23
-
View All
-
11 May, 2023REPORT BY THOSE CHARGED WITH GOVERNANCE AND CONSOLIDATED FINANCIAL STATEMENTS FOR THE YEAR ENDED 30TH JUNE, 2022
-
25 Oct, 2022Financial statements and compliance audit of public debt and general service (vote 22) for the financial year ended 30 June 2021
-
25 Oct, 2022Financial statements of public debt and general services (vote 22) for the financial year ended 30 June, 2020
-
25 Oct, 2022Financial statements of public debt and general services (vote 22) for the financial year ended 30 June, 2019
-
10 Jun, 2022CONSOLIDATED FINANCIAL STATEMENTS 30 JUNE 2021
-
03 Mar, 2022Audited Consolidated Financial Statements for the year ended 30th June, 2020"
-
02 Mar, 2022Audited Consolidated Financial Statements for the year ended 30th June, 2019"
-
28 Feb, 2022Audited Consolidated Financial Statements for year ended 30th June, 2018
-
27 Feb, 2022Audited Consolidated Financial Statements for year ended 30th June, 2017
-
View All
-
06 Nov, 2024UFANISI WA MIFUKO NA PROGRAMU ZA SERIKALI ZA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
-
06 Nov, 2024MATOKEO YA HUDUMA ZA UWAKALA WA BENKI KATIKA UKUAJI WA SEKTA NDOGO YA BENKI TANZANIA
-
View All
-
17 Feb, 2023Enhanced-SP-Portal-User Manual
-
17 Feb, 2023GePG-Helpdesk-User-Manual
-
17 Feb, 2023GePG-LUKU-Portal-User-Manual
-
17 Feb, 2023GePG-POS-APP-USER-MANUAL
-
17 Feb, 2023GEPG-RECONCILIATION-TOOL-USER-MANUAL
-
View All
-
13 Jun, 2025ECONOMIC SURVEY CITIZEN VERSION 2024
-
12 Jun, 2025HALI YA UCHUMI WA TAIFA 2024
-
13 Jun, 2024HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2023
-
28 Jul, 2023ECONOMIC SURVEY REPORT -2023-24
-
15 Jun, 2023ECONOMIC SURVEY 2023
-
14 Jun, 2023ECONOMIC SURVEY 2022.
-
14 Jun, 2023KITABU_CHA_HALI_YA_UCHUMI_WA_TAIFA_KATIKA_MWAKA_2022
-
14 Jun, 2022HALI YA UCHUMI WA TAIFA 2021
-
12 Jun, 2022Hali ya Uchumi wa Taifa 2020
-
28 Feb, 2022HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2018
-
View All
-
21 May, 2024MAREKEBISHO YA KANUNI ZA PPP 2023
-
21 May, 2024MAREKEBISHO YA SHERIA YA PPP, 2023
-
21 May, 2024MKAKATI WA UTEKELEZAJI WA SERA YA PPP
-
15 May, 2022Approved PPP Regulations, 2020
-
15 May, 2022PPP ACT RE 2018
-
15 May, 2022PPP Policy 2009
-
View All
DKT. NCHEMBA AWASISITIZA WATUMISHI KUSIMAMIA UCHUMI.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alipowasili kwa ajili ya kuhudhuria katika kikao cha wafanyakazi wa Wizara yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaagiza viongozi na watumishi wa Wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uaminifu ili kuendelea kusimamia uchumi wa nchi.
Ametoa agizo hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali, Mtumba, wakati wa Kikao cha watumishi wa Wizara hiyo ambacho kinatoa fursa kwa watumishi kukutana kwa pamoja, kukumbushana na kubadilishana uzoefu, taarifa na uelewa kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Serikali kwa ujumla.
Dkt. Nchemba aliwakumbusha watumishi hao kutambua kuwa Wizara ya Fedha ni moyo wa Serikali hivyo ikiyumba tu nchi itayumba na kuleta madhara kijamii na kiuchumi.
Aliwasisitiza waendelee kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano pamoja na kufanya marekebisho katika maeneo yenye changamoto ili kuboresha utendaji wao na kufikia malengo yaliyowekwa.
”Tutumie kikao hiki kurekebisha maeneo yote yenye changamoto, hakuna binadamu aliyekamilika na ukijiona mkamilifu ujue unamkufuru Mwenyezi Mungu, hivyo inabidi tukubali kubadilika ili kuboresha utendaji wetu”, Alisisitiza Dkt. Nchemba.
Aidha, aliwapongeza watumishi hao kwa kufanya kazi kwa weledi na kuiwezesha nchi kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na kuhimili changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazoendelea ulimwenguni.
’’Mmekuwa mstari wa mbele kuliwezesha Taifa kuhimili misukusuko ya kiuchumi chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na usimamizi imara wa uchumi unaendelea licha ya misukosuko inayoendelea duniani’’, alibainisha Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa utendaji wa watumishi wa Wizara hiyo umeiwezesha nchi kutekeleza miradi ya maendeleo lakini pia kuwaongezea sifa binafsi Waziri na Naibu wake Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb).
Dkt. Nchemba alisema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo watumishi ili waweze kufanya vizuri zaidi katika majukumu yao na kuiwezesha nchi kufikia malengo yake.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, aliwaasa Watumishi wa Wizara hiyo kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mapato na matumizi ya mali na fedha za umma ili kufikia malengo ya Serikali katika mwaka wa fedha 2025/26.
Alisema ni muhimu kwa watumishi hao kutumia weledi na uzoefu walionao kuongeza tija katika usimamizi wa sera, sheria, kanuni na miongozo ya masuala ya fedha na bajeti ili kuwezesha Wizara kutekeleza kwa ufanisi malengo yake na Serikali kwa ujumla.
”Ninapenda kuwakumbusha watumishi wote kutekeleza majukumu yetu kwa kuzingatia malengo, shabaha na mpango na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge pamoja na kutunza siri na kuhifadhi nyaraka muhimu za Wizara na Serikali kwa ujumla”, alisisitiza Dkt. Mwamba.
Aliwataka Wakuu wa Idara/Vitengo pamoja na watumishi wote kuzingatia maelekezo hayo kwa ukamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo alisisitiza umuhimu wa kufanyakazi kwa upendo, umoja na mshikamano pamoja na kuendelea kusimamia maadili ya kazi ili kuwezesha wote kufikia malengo yao.
”Wote tunategemeana hakuna mtu anayejua kila kitu, hivyo ni muhimu kupeana nafasi ya kuweza kufikia mafanikio yetu, hakuna mtu anayeweza kufanikiwa bila kuwezeshwa”, alisisitiza Bi. Omolo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Usimamizi wa Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya, aliwapongeza watumishi wa Wizara hiyo kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa majukumu yao.
Alisema watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa moyo, kujitolea na kukesha kuhakikisha shughuli mbalimbali za Serikali zinatekelezwa kwa wakati na kwa mafanikio makubwa.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayesimamia Fedha za Umma, Bi. Amina Khamis Shaaban alisisitiza Wizara hiyo kuendelea kusimamia ukusanyaji wa fedha za ndani ili kuwezesha nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha alihimiza watumishi wa Wizara hiyo kusimamia upatikanaji wa mikopo nafuu ili kuiwezesha nchi kutumia fedha hizo kama kichocheo cha kujenga uwezo wa ndani na kujinasua kwenye utegemezi wa muda mrefu.
Bi. Amina aliongeza kuwa katika kupunguza utegemezi huo suala la Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) ni muhimu, na kusisitiza watumishi wa Wizara hiyo hususan wale wanaohusika na PPP kuibua na kusimamia kikamilifu miradi ya ubia.
Kwa upande wao Mhasibu Mkuu wa Serikali CPA (T), Leonard Mkude na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Bw. Benjamin Magai, walisema kuwa ushirikiano uliotolewa na watumishi umewezesha wizara kukamilisha majukumu ya kimalipo katika mwaka wa fedha 2024/25.
Aidha, waliongeza kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo imeweza kutekelezwa pamoja na kukamilisha ufuatiliaji na tathmini katika miradi hiyo.
Katika kikao hicho viongozi walihimiza utulivu, uwajibikaji, uadilifu, kutunza siri na mali za umma pamoja na kujilinda katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Serikali huku wakisisitiza watumishi hao kushiriki zoezi hilo kikamilifu kwa maslahi mapana ya nchi.
Mwisho.