Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA ATETA NA WAZIRI WA FEDHA WA KONGO KUHUSU UJENZI WA RELI YA KISASA-SGR

20 Jul, 2023
DKT. NCHEMBA ATETA NA WAZIRI WA FEDHA WA KONGO KUHUSU UJENZI WA RELI YA KISASA-SGR
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt  Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kulia, akisalimiana na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Mhe. Nicolas Kazadi, walipokutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Kinshasa nchini DRC, kuhusu mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaotarajiwa kujengwa kutoka Uvinza nchini Tanzania hadi Gitega nchini Burundi kupitia Musongati kwenye machimbo ya madini na kipande kingine cha reli kinachokusudiwa kufika KINDU nchini DRC kupitia Uvira kwenye mpaka wa Burundi na DRC. 
 
Waziri wa Fedha. Mhe. Dkt.  Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Nicolas Kazadi, kuhusu mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza nchini Tanzania hadi Gitega nchini Burundi kupitia Musongati kwenye machimbo ya madini na kipande kingine cha reli kinachokusudiwa kufika KINDU nchini DRC kupitia Uvira kwenye mpaka wa Burundi na DRC.
 
Mazunguzo hayo yamefanyika mjini Kinshara, Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, kando ya mkutano  wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa jopo la mapitio ya uchumi mpana katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
 
“Nia ya Tanzania katika utekelezaji wa mradi huo ni kuunganisha Nchi ya Burundi na Congo kwenye soko la dunia kupitia bandari ya Dar es Salaam, katika utekelezaji wa mradi huo wa Reli ili kukuza biashara,” alisema Dkt. Nchemba
 
 Alisema kuwa Tanzania inajenga awamu ya kwanza ya reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa kutoka Dar es salaam hadi Mwanza kupitia Tabora yenye urefu wa kilomita 1,219 ambayo imegawanywa katika sehemu tano. 
 
Dkt. Nchemba alifafanua kuwa Serikali ya Tanzania iko katika maandalizi ya kujenga kipande cha kutokea Tabora hadi Kigoma kupitia Uvinza chenye urefu wa kilometa 411, na tayari mchakato wa manunuzi ya mkandarasi wa kusanifu na kujenga umekamilika.
 
Akizungumzia mambo muhimu kwenye upatikanaji wa fedha, Dk Nchemba alisema Tanzania imeiomba rasmi Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kupitia madirisha yake ya ADB na ADF kusimamia upatikanaji wa mkopo kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa njia ya reli ya Standard Gauge kwa kipande (lot) cha  cha  sita kutoka Tabora – Uvinza chenye urefu wa 411km  na loti  ya saba kutoka Uvinza – Malagarasi, km 156.
 
 Dk Nchemba alisema ujenzi wa loti ya kwanza kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro umefikia asilimia 98.14 wakati loti  ya pili  kutoka Morogoro hadi Makutopora umefikia asilimia 93.83.
 
Loti ya tatu  kutoka Makutopora hadi Tabora umefikia asilimia 7.0 na loti ya nne kutoka Tabora hadi Isaka asilimia 2.39 na Ujenzi wa loti ya tano  kutoka Mwanza  hadi Isaka umefikia asilimia 31.07.
 
Kwa upande wake Waziri wa fedha wa DRC Congo, Mhe. Nicolas Kazadi alisema kuwa mradi huo ni mhimu kwa nchi yake na kwamba kukamilika kwake kutaongeza fursa za kiuchumi na kuchochea maendeleo ya nchi na washirika na kuongeza kuwa pamoja na Reli, alitaka kuwepo juhudi za makusudi za kuboresha miundombinu ya Barabara na Bandari ya Kalemie.
 
Mwisho.