Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR

21 Mar, 2024
DKT. NCHEMBA ATETA NA UONGOZI WA BENKI YA WATU WA ZANZIBAR
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza wakati wa Kikao chake na Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Katika Ukumbi wa Waziri wabFedha, Jijini Dodoma, ambapo walijadili namna Benki na Serikali zinaweza kushirikiana kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali na PBZ.
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kupanua biashara zake hapa nchini na kuitaka Benki hiyo ishushe zaidi riba ili wananchi wakiwemo watumishi wa Umma waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na Benki hiyo.
 
Dkt. Nchemba ameyasema hayo alipokutana na Uongozi wa Benki hiyo Ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo walijadili namna Benki na Serikali zinaweza kushirikiana kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
 
Aliahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za Benki hiyo kwa kuhakikisha kuwa wananufaika na mazingira ya ufanyaji biashara katika Sekta hiyo ya fedha.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Benki hiyo, Bw. Said Mohamed Said, alisema kuwa Benki yake imeendelea kukua na kupanua huduma zake upande wa Tanzania Bara, katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Dodoma na kwamba hivi karibuni inatarajia kufungua matawi mengine katika mikoa ya Mbeya, Morogoro, Mwanza, Tanga na Arusha.
 
Bw. Said alisema kuwa Benki yake imeendelea kukua na katika kipindi cha miaka mitatu sasa ilipata faida ya shilingi bilioni 75 kabla ya kulipa kodi, ina mali zisizohakishika zenye thamani ya shilingi trilioni 2 na katika kipindi hicho imetoa mikopo inayofikia zaidi ya shilingi bilioni 194.
 
Aliniomba Wizara ya Fedha iisaidie Benki hiyo iingizwe kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya kielektroniki wa GePG, kwa ajili ya kukusanya malipo ya Serikali na kuangalia namna ya kupunguza baadhi ya gharama ili waendelee kutoa mikopo kwa riba nafuu kwa wateja wao kama ilivyodhamira ya Benki hiyo inayomilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Mwisho