Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA BODI YA BENKI KUU YA TANZANIA- BOT

20 Jun, 2025
DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA BODI YA BENKI KUU YA TANZANIA- BOT

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ukiongozwa na Gavana wa Benki hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba (wa nne kulia), ambapo  walieleza kuhusu mafanikio ya Benki hiyo likiwemo suala la kuendelea kuimarisha uchumi wa nchi, jijini Dodoma.

 

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ukiongozwa na Gavana wa Benki hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba, ambapo umeangazia mafanikio ya Benki hiyo katika kuendelea kuimarisha uchumi.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, Dkt. Nchemba aliitaka Bodi hiyo ya Benki Kuu ya Tanzania kuendelea kusimamia misingi iliyoanzisha Bodi hiyo.

Alisema kuwa Wizara ya Fedha itaendendelea kutoa ushirikiano kwa Bodi hiyo ili kuendelea kuimarisha uchumi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Gavaa wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, alisema kuwa Benki Kuu imeendelea kufanya vizuri katika kuimarisha uchumi na hilo linadhihirika baada ya nchi kupitia vipindi tofauti vya msukosuko wa uchumi uliozikumba pia nchi nyingi Duniani.

Mwisho.