Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. NATU MWAMBA ATETA NA UONGOZI WA AFDB

22 Oct, 2025
DKT. NATU MWAMBA ATETA NA UONGOZI WA AFDB

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bw Ronald Justin Cafrine,  ripoti ya utekelezaji wa shughuli za TADB kwa miaka 10 (TADB 10 years Impact Report), tukio lilofanyika katika Ubalozi wa Tanzania, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jijini Washington D.C, nchini Marekani.

AfDB ni mdau Mkuu wa Serikali ambapo kupitia Benki hiyo, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kupitia Serikali, kwa nyakati tofauti, kati ya mwaka 2021 na 2024, ilipokea kiasi cha shilingi bilioni 382 kwa ajili kuimarisha mtaji ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo na uchumi kwa wananchi

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB), Bw. Frank Nyabundege, alieleza kuwa AfDB imeahidi kuipatia TADB kiasi kingine cha takribani USD  60m mwaka 2026 kwa ajili ya kuimarisha zaidi mtaji.

Dkt. Natu Mwamba, anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayofanyika Washington D.C, nchini Marekani.