Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MWAMBA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

06 Jun, 2025
DKT. MWAMBA ATETA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiagana na Kiongozi Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bi. Abha Prasad, baada ya kumalizika kwa kikao kazi kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao hicho  kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo, kikao ambacho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Katika kikao hicho wamejadiliana kuhusu kuendeleza mageuzi ya kimfumo yanayolenga uthabiti wa kiuchumi, uboreshaji wa fedha za umma, uhimilivu wa deni la serikali, kukuza sekta binafsi katika ujumuishaji wa kijamii katika masuala ya kiuchumi na uangalizi wa mabadiliko ya tabianchi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Kamishna wa Idara Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Japhet Justine, Kamishina wa Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Serikali, Wizara ya Fedha, Bw. Nuru Ndile na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya Dunia.

MWISHO