Category Title

  • Government Budget Speeches
  • Ministry's Budget Speeches
  • Budget Books 2024/2025
  • Budget Books 2023/2024
  • Budget Books 2022/2023
  • Budget Books 2021/2022
  • Budget Books 2020
  • Budget Books 2018/2019
  • Budget Books 2015/2016
  • Budget Books 2014/2015
  • Content not found
  • Content not found
  • Content not found

DKT. MWAMBA AKIPONGEZA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI KWA UTENDAJI MZURI

11 Mar, 2025
DKT. MWAMBA AKIPONGEZA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI KWA UTENDAJI MZURI
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akikabidhiwa Jarida la ‘’Hazina Yetu’’ Toleo la Pili kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, na Naibu Katibu Mkuu, anayesimamia Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Christian Omolo (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, ofisini kwake, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo amekipongeza Kitengo hicho kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutangaza na kuhabarisha umma kuhusu Sera, Program, Mikakati na Mipango mbalimbali inayofanywa na Wizara katika kusimamia uchumi wa nchi.


 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba, amekipongeza Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Wizara hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhabarisha umma kuhusu kazi na majukumu ya Wizara katika kukuza na kusimamia uchumi kwa njia mbalimbali za mawasiliano
 
Dkt. Mwamba ametoa pongezi hizo jijini Dodoma wakati akipokea Jarida la Pili la liitwalo Hazina Yetu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 linaloandaliwa na Kitengo hicho kila baada ya miezi mitatu.
 
Dkt. Mwamba alisema kazi za Kitengo hicho zinajieleza kwa kuwa amekuwa akipokea pongezi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali wanaofutilia mitandao ya kijamii ya Wizara pamoja na vyanzo vingine vya habari ambapo aliahidi kuendelea kukijengea uwezo Kitengo hicho ili kiweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
 
“Asanteni sana, kwakweli mnatuheshimisha viongozi wenu, mnafanya kazi nzuri naomba muendelee kufanya kazi kwa bidii”, alisisitiza Dkt. Mwamba.
 
Aidha, alipongeza Jarida alilolipokea kwa kuwa na muonekano mzuri wenye mpangilio mzuri wa makala, habari na picha ambazo zinavutia kuzitazama na kuzisoma.
 
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bi. Jenifa Chistrian Omolo alisema Kitengo hicho kimekuwa kikitoa taarifa kwa wakati na kuwawezesha wananchi kujua matukio mbalimbali yanayoendelea Wizarani kwa mustakabali wa nchi.
 
Alisema taarifa hizo zimetengeneza taswira ya Wizara kwa jamii kwa kuwa wananchi wengi wameweza kujua majukumu na kazi mbalimbali zinazotekelezwa ikiwa ni pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa imara.
 
Akipokea pongezi hizo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, aliwashukuru viongozi hao kwa kuona mchango wa Kitengo katika Wizara na kutoa ushirikiano mkubwa  na kuahidi kuongeza juhudi zaidi ili kuhakikisha wananchi wanasikia mafanikio ya Serikali kupitia Wizara hiyo.
Mwisho.